KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Friday, December 14, 2012

SAFARI YA MTANZANIA TEMBELEA TANZANIA KUANZA KESHO




KAMPUNI ya Lakeland Africa kesho itaanza safari ya ‘Mtanzania tembelea Tanzania’ kwa siku 14 kwa lengo la kukuza utalii wa ndani na kujenga utamaduni wa Watanzania kutembelea vivutio vya utalii nchini.

Safari hiyo itakayoanzia Mlimani City Dar es Salaam kesho inatoa fursa kwa watanzania kutembelea vivutio mbalimbali ikiwemo Hifadhi ya Saadan, Pangani, Lushoto, Tarangile, Olduvai Gorge, Lake Manyara, Ngorongoro na Serengeti na pia watapata nafasi ya kutembelea kijiji cha Butiama alikozaliwa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Nyerere na kuzuru katika kaburi lake.

“Lakeland Africa sasa itaendesha safari za namna hii kuhimiza watu kutembelea vivutio vya utalii nchini kwa kauli mbiu ya ‘kuwa mtalii ndani ya nchi yako”

Kuanzia mwezi Januari mwakani Lakeland Africa itaendesha safari za kila wiki kwenda hifadhi na makumbusho ya kistoria katika maeneo mbalimbali hapa nchini ikiwamo Lushoto, Pangani, Saadani, Selous, Kilwa, Bagamoyo na Mikumi

Katika kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anapata fursa hii ya kuitembelea nchi yake Lakeland Africa imeandaa ratiba ya mwaka mzima ya safari zote ili watu waweze kuchagua na kupanga safari kulingana mahitaji yao.

Wapigie Lakeland Africa sasa kupanga safari yako ya mwakani, mwezi wowote utaopenda kuzuru na kuwa mtalii ndani ya nchi yako.

Imetolewa na Lakeland Africa.
+255222-761811
+255784885901
Email: reservations@lakelandafrica.com
www.lakelandafrica.com
‘Kuwa mtalii ndani ya nchi yako’

No comments:

Post a Comment