KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, December 27, 2012

MTEMVU AMPIGA JEKI DOGO ASLAY DOLA 1,200



MBUNGE wa jimbo la Temeke kwa tiketi ya CCM, Abbas Mtevu amempatia msanii Dogo Asley wa kundi la TMK Wanaume Family, dola 1,200 kwa ajili ya safari yake ya kwenda Ivory Coast.

Aslay amekabidhiwa kiasi hicho cha fedha na msaidizi wa mbunge huyo katika hafla iliyofanyika ofisini kwake, Temeke, Dar es Salaam.

Msaidizi huyo wa mbunge alisema bosi wake ameamua kumpatia Aslay kiasi hicho che fedha ili kutimiza ahadi aliyoitoa wakati wa mkutano mkuu wa CCM uliofanyika Novemba mwaka huu mjini Dodoma.

Akipokea fedha hizo, Aslay alimshukuru mbunge huyo kwa kutimiza ahadi yake na kuwataka watanzania wamwombee dua ili aweze kufanya vizuri katika tuzo.

Sherehe za utoaji tuzo za Kora kwa wanamuziki bora barani Afrika, zimepangwa kufanyika keshokutwa mjini Abidjan, Ivory Coast.

Aslay ameteuliwa kuwania tuzo ya msanii mpya anayechipukia kupitia wimbo wake wa Niwe Nawe. Aslay anapambana na wasanii kutoka nchi nyingine kama Uganda, Burkina Faso, Zambia, Nigeria na Afrique Du Sud.

Mbali na Dogo Aslay, wasanii wengine kutoka Tanzania walioteuliwa kuwania tuzo hizo ni Lady Jay Dee, Saida Karoli na Ali Kiba.

No comments:

Post a Comment