KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, December 6, 2012

TAIFA QUEENS YANUSA UBINGWA SINGAPORE




TIMU ya taifa ya netiboli, Taifa Queens imeukaribia ubingwa wa michuano ya kimataifa ya mchezo huo inayoendelea nchini Singapore baada ya kuingia fainali bila kufungwa.
Taifa Queens imebakiwa na mchezo mmoja dhidi ya Namibia, uliotarajiwa kuchezwa jana jioni, ambapo kati ya timu sita zinazoshiriki mashindano hayo, ndiyo pekee, ambayo haijafungwa.
Katika mchezo wa jana, Taifa Queens ilicheza dhidi ya wenyeji Singapore na kuibuka na ushindi wa mabao 51-34.
Iwapo Taifa Queens itaifunga Namibia katika mechi yake ya mwisho, itakuwa imeweka rekodi ya kutofungwa katika mashindano hayo, ambayo inatarajiwa kufungwa leo.
Michuano hiyo imeandaliwa na Chama cha Netiboli cha Singapore na kusimamiwa na Shirikisho la Kimataifa la Netiboli (IFNA).

No comments:

Post a Comment