KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, December 13, 2012

KOFFI OLOMIDE ATUA DAR



Mwanamuziki nyota wa dansi kutoka nchini DRC-Kongo,Koffi Olomide akiwasalimia baadhi ya mashabiki wake waliofika kumlaki usiku wa kuamkia leo mara baada ya kuwasili akiwa sambamba na skwadi lake zima la Quartier Latin kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA),tayari kwa onesho lake litakalofanyika siku ya jumamosi ndani ya viwanja vya Lidaz Club,Kinondoni jijini Dar na jumapili jijini Mwanza ndani ya uwanja wa CCM-Kirumba,onesho hilo ambalo limedhaminiwa na kampuni ya bia ya Afrika Masharikia (EABL) kupitia kinywaji chake cha Tusker kiingilio chake kimepangwa kuwa ni shilingi 10,000/= kwa kichwa kama tiketi ikinunuliwa mapema na shilingi 15,000/= getini.
Watangazaji wa Clouds FM na Clouds TV pichan shoto ni Millard Ayo na Ben Kinyaiya pichani kulia wakifanya mahojiano mafupi na Mwanamuziki Koffi Olomide mara baada ya kuwasili usiku wa kuamkia leo  kwenye uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA),jijini Dar.Koffi alitanabaisha kuwa yeye amekuja nchini Tanzania kwa mara nyingine tena kuwaburudisha na kuwaonesha vipaji alivyo navyo sasa ndani ya kundi lake la Quartier Latin.
MKURUGENZI wa Prime Time Promotions, Joseph Kusaga akimlaki mwanamuziki Koffo Olomide mara baada ya kutua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo
Wacheza shoo wa kundi la Quartie Latin linaloongozwa na Koffi Olomide wakiwa nje ya hoteli ya Serena

No comments:

Post a Comment