KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, December 3, 2012

LULU AENDELEA KUSOTA LUPANGO


UPELELEZI wa kesi ya mauaji inayomkabili msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael ‘Lulu’, haujakamilika.
Lulu (17), anadaiwa kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba, Aprili 7, mwaka huu, eneo la Sinza Vatican, Dar es Salaam.
Mshitakiwa huyo leo alipandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Augustina Mmbando.
Wakili wa Serikali, Keneth Sekwao alidai kesi hiyo ilifikishwa mahakamani hapo kwa ajili ya kutajwa na kwamba upelelezi bado haujakamilika.
Semkwao aliiomba mahakama hiyo tarehe nyingine ya kutajwa kwa kesi hiyo. Hakimu Augustina alisema kesi hiyo itatajwa Desemba 17, mwaka huu.
Kwa mujibu wa hati ya mashitaka , Lulu anadaiwa Aprili 7, mwaka huu, eneo la Sinza Vatican, Dar es Salaam, mshitakiwa alimuua Kanumba.
Kanumba alizikwa Aprili 10, mwaka huu, kwenye makaburi ya Kinondoni, katika mazishi ambayo yalihudhuriwa na maelfu ya watu wakiwemo viongozi wa serikali.

No comments:

Post a Comment