KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, December 24, 2012

AZAM BINGWA KOMBE LA UHAI




 Mwenyekiti mstaafu wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Kanali mstaafu Idd Kipingu akimkabidhi nahodha wa timu ya Azam FC, Abdul Mgaya kombe la Ubingwa wa  michuano ya Uhai Cup 2012 baada ya timu hiyo kuifunga Coastal Union ya Tanga kwa penalti 3-1 katika mchezo wa fainali ya vijana chini ya miaka 20 uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam. Katikati ni Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Leodgar Tenga. (Picha zote na Habari Msetoto Blog)

TIMU ya soka ya vijana wa chini ya umri wa miaka 20 ya Azam imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Kombe la Uhai baada ya kuishinda Coastal Union kwa penalti 3-1.

Mshindi wa pambano hilo ilibidi apatikane kwa njia ya matuta baada ya timu hizo kumaliza dakika 120 zikiwa sare ya mabao 2-2.

Katika michuano hiyo, Bakari Shime wa Coastal Union ametwaa tuzo ya kocha bora, Mansur A. Mansur wa Coastal Union kipa bora, Ramadhan wa Simba aliyefunga mabao sita, ameibuka mfungaji bora, Ruvu Shooting timu yenye nidhamu, Joseph Kimwaga wa Azam mchezaji bora na Isiaka Mwalile refa bora.

No comments:

Post a Comment