KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Friday, June 30, 2017

DIAMOND AFANYA UZINDUZI WA BIDHAA YAKE MPYA YA KARANGA






MSUVA AIPELEKA ROBO FAINALI COSAFA ‘TAIFA STARS’



Timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’ imetinga hatua ya  Robo Fainali ya michuano ya Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika (COSAFA) Castle baada ya sare ya 1-1 na Mauritius jioni ya leo Uwanja wa Moruleng mjini Rusternburg, Afrika Kusini.

 Simon Msuva aliyetokea benchi kipindi cha pili na kwenda kuifungia Taifa Stars bao la kusawazisha dakika ya 68, dakika moja tu baada ya Kevin Perticots aliyetokea benchi pia kuifungia bao la kuongoza Mauritius.

Kwa matokeo hayo, Tanzania inaungana na Botswana, Zambia, Afrika Kusini, Namibia, Lesotho na Swaziland zilizoanzia hatua hiyo na watamsubiri mshindi wa Kundi B kesho kukamilisha ‘Nane Bora’ za COSAFA 2017.

Na hiyo ni baada ya kumaliza na pointi tano sawa na Angola, lakini Taifa Stars inabebwa na wastani wake mzuri wa mabao, huku Mauritius na Malawi zote zikimaliza na pointi mbili kila moja.

Kundi B hadi sasa, Zimbabwe inaongoza kwa wastani wa mabao tu, ikiwa na pointi nne sawa na Madagascar, wakati Msumbiji ina pointi tatu na Shelisheli haina kitu.  

Mauritius leo ilimaliza pungufu baada ya mchezaji wake, Damien Balisson kutolewa kwa kadi nyekundu dakika ya 78, lakini Tanzania ikashindwa kutumia mwanya huo kuongeza mabao.

Kikosi cha Tanzania kilikuwa; Aishi Manula, Hassan Kessy, Gardiel Michael, Abdi Banda, Salim Mbonde, Erasto Nyoni, Himid Mao, Shiza Kichuya, Elias Maguri/Simon Msuva dk58 na Thomas Ulimwengu.

WAGOMBEA 29 WAFANYIWA USAILI TFF



Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limefanya usaili kwa wagombea 29 wa nafasi mbalimbali katika siku ya kwanza ya hatua hiyo muhimu kuelekea uchaguzi mkuu wa shirikisho.

Kabla ya usaili, Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Revocatus Kuuli, aliwatangazia wagombea wote kuwa amepokea mapingamzi mawili ambayo ni:-

Hussein Mwamba ambaye ni Mjumbe kwa sasa wa Kamati ya Utendaji ya TFF, aliyempinga Mussa Sima kuwa amejitokeza kuwania nafasi hiyo katika Kanda ya 10 ya Mikoa ya Dodoma na Singida kuwa hana uzoefu wa miaka mitano.

Wanafamilia wote kwa maana ya Mwamba na Sima walikuwako. Wakaitwa kikaoni, lakini mweka pingamizi – Mwamba aliamua kulitoa pingamizi lake.

Pingamizi jingine ambalo liliwekwa leo ni kwa Mgombea nafasi ya urais John Kijumbe ambaye anapinga Wallace Karia – Makamu Rais kwa sasa wa TFF kwamba hana sifa za kuwania urais wa TFF kama alivyoomba.

Hata hivyo, pingamizi hilo halijasikilizwa kwa sababu ya wahusika wote kutokuwako na baada ya kamati kufanya nao mawasiliano, wametangaza kusikiliza pingamizi hilo Jumamosi ambayo ni siku ya mwisho ya usaili.

Wagombea ambao wamesailiwa leo hadi jioni ya leo Alhamisi kwa upande wa wagombea urais ni Imani Madega na Ally Mayay wakati Wagombea Makamu urais waliosailiwa ni Mtemi Ramadhani na Mulamu Nghambi.

Kanda Na. 1 Mikoa ya Kagera na Geita;

Soloum Chama

Kaliro Samson

Leopold Mukebezi

Kanda Na. 2 Mikoa ya Mara na Mwanza;

Aaron Nyanda

Samwel Daniel

Bado

Vedastus Lufano

Ephraim Majinge

Kanda Na. 3 Mikoa ya Shinyanga na Simiyu;

Mbasha Matutu

Bado

Benista Rugora

Stanslaus Nyongo

Kanda Na. 4 Mikoa ya Arusha na Manyara;

Wote Bado

Omari Walii

Sarah Chao

Peter Temu

Kanda Na. 5 Mikoa ya Kigoma na Tabora;

John Kadutu

Bado

Issa Bukuku

Abubakar Zebo

Francis Michael

Kanda Na. 6 Mikoa ya Katavi na Rukwa;

Baraka Mazengo

Bado

Kenneth Pesambili

Kanda Na. 7 Mikoa ya Mbeya, Songwe na Iringa;

Elias Mwanjala

Cyprian Kuyava

Bado

Erick Ambakisye

Abousuphyan Silliah

Kanda Na. 8 Mikoa ya Njombe na Ruvuma;

Wote bado

James Mhagama

Golden Sanga

Vicent Majili

Yono Kevela

Kanda Na. 9 Lindi na Mtwara;

Wote Bado

Athuman Kambi

Dunstan Mkundi

Kanda Na. 10 Mikoa ya Dodoma na Singida;

Hussein Mwamba

Mohamed Aden

Musa Sima

George Benedict Komba

Bado

Stewart Masima

 Ally Suru

Kanda Na. 11 Mikoa ya Pwani na Morogoro;

Gabriel Mkwawe

Bado

Charles Mwakambaya

Francis Ndulane

Hassan Othman ‘Hassanol’

Kanda ya 12. Mikoa ya Kilimanjaro na Tanga

Khalid Mohamed

Bado

Goodluck Moshi

Thabit Kandoro

Kanda Na. 13 Mkoa wa Dar es Salaam

Emmanuel Ashery

Shaffih Dauda

Mussa Kisoky

Lameck Nyambaya

Jamhuri Kihwelo

Saad Kawemba

Bado

Bakari Malima

Ayoub Nyenzi

Saleh Alawi

Ramadhani Nassib

 Aziz Khalfan

Abdul Sauko

Peter Mhinzi

Ally Kamtande

Said Tully

MAKOCHA 19 WAFUZU KOZI YA DARAJA A YA CAF


Makocha 19 wa mpira wa miguu, wamehitimu kozi ya Daraja ‘A’ ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) iliyofanyika Makao Makuu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), iliyoko Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

Makocha hao walimaliza gwe ya pili ya siku 19, katika kozi hiyo ambayo mbali ya kuwa na wakufunzi wengine, wakufunzi wakuu wa CAF walikuwa ni Athumani Lubowa na Sunday Kayuni.

Kayuni ambaye ni Mkurugenzi wa zamani wa TFF katika kozi hii amehudumu kama mkufunzi mkuu wa CAF na aliyekuja kuwasimamia (Accessor) ni Mkurugenzi wa sasa wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Uganda, Athumani Lubowa.

Makocha waliohitimu ni Kidao Wilfred Mzigama, Ali Vuai Shein, Wane Nelson Mkisi, Abdulmutik Haji Ali, Hababuu Ali Omar, Meck Maxime Kianga, Salim Ali Haji, Malale Hamsini Keya na Abdallah Mohammed Juma.

Wengine ni Salim Juma Makame, Emmanuel Raymond Massawe, Mohammed Alawdin Tajdin, Fikiri Elias Mahiza, Juma Ramadhani Mgunda na Dismas Gordon Haonga, Abdul Hassan Banyai, Maka Andrew Mwalwisi, Dennis Mrisho Kitambi na Sebastian Leonard Nkoma.

Akifunga kozi hiyo, Mgeni rasmi Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa TFF, Khalid Mohammed Abdallah aliwatakia kila la kheri kwa makocha hao akiwaelezea kuwa wamejaa utajiri wa ufundi ambao hawana budi kuutendea haki kwa kuibua, kukuza na kuendeleza vipaji vya mpira wa miguu.

Awali, akizungumzia wahitimu hao, Mkufunzi Lubowa alisema kwamba anamini makocha hao watafanya vema kwa kuwa katika kipindi chote cha kozi, walionyesha kuwa na nidhamu ya hali ya juu – alama kuu ya mafanikio.

MALINZI, MWESIGWA WAPELEKWA RUMANDE HADI JULAI 3; AVEVA, KABURU HADI JULAI 13





Rais wa TFF, Jamal Malinzi hataweza kutetea kiti chake cha urais kwa kuwa amepelekwa mahabusu katika Gereza la Segerea baada ya kukosa dhamana hadi Jumatatu Julai 3 kesi yake itakaposikilizwa tena.

Malinzi pamoja na Katibu wake, Mwesigwa Celestine wanashitakiwa kwa makosa 28 yakiwemo ya kugushi na utakatishaji fedha.

Wote wawili wamepandishwa gari kwenda Segerea hadi Jumatatu kesi yao itakaposikilizwa tena.

Pamoja na wao, Rais wa Simba,  na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ wanaoshitakiwa kwa makosa ya utakatishaji, nao wamechukuliwa kupelekwa Segerea.

Kaburu na Aveva watakuwa mahabusu hadi Julai 13 baada ya kukosa dhamana kutokana na kesi inayowakabili.

Baada ya mahakama ya hakimu mkazi Kisutu kuwanyima dhamana Rais wa TFF Jamal Malinzi, Katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa na afisa wa fedha Nsiande Mwanga, jopo la mawakili wa utetezi wameonekana kutoridhika na wateja wao kukosa dhamana.

“Washtakiwa kukamatwa na kufikishwa mahakamani halafu wanaomba tena upelelezi wa kesi wakati suala tayari lipo mahakamani hiyo ndio pointi kubwa ambayo tumeiibua halafu kitu kingine tulichokiibua ni pamoja na maombi ya dhamana,”  Jarome Msemwa-wakili upande wa utetezi.

“Tumeiomba mahaka itoe dhamana kwa wateja wetu, kuna sheria ya Bunge inayokataza dhamana halafu kuna katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoruhusu dhamana. Kwa hiyo kwa amri ya mahakama ambayo imesomwa leo (jana) wateja wetu wanapelekwa rumande hadi Jumatatu Julai 3, 2017.”

“Sikutarajia katika muda na wakati kama huu kutakuwa na mashitaka yanayowakabili yanayofika 28 ya aina ileile lakini ndani yake yanatengenezwa machache kufanywa ya tutakatisha fedha wakati mashitaka yote tunayaona ni kughushi na kila kitu wanacho. Mimi sikutegemea kama watasema upelelezi haujakamilika wakati uchunguzi wao wamesema ni wa muda mrefu sana,” Aloyce Komba-wakili upande wa utetezi.

“Mvutano ulikuwa ni wa kisheria ambapo mwisho wa siku mahakama ikabidi ifanye maamuzi, sisi tulikuwa tunaomba dhamana vilevile kesi ianze kusikilizwa na tulikuwa tunasema hawawezi kusema upelelezi bado haujakamilika wakati wameshakamilisha kilakitu. Vilevile tukataka mtazamo huu ubadilike hapa nchini wa kuwaleta watu mahakamani halafu uchunguzi bado haujakamilika wanaishia kukaa ndani.”

Watuhumiwa wote walikana mashitaka yote 28 yanayowakabali hivyo kesi hiyo kuahirishwa hadi Jumatatu Julai 3, 2017.

Thursday, June 29, 2017

MALINZI, MWESIGWA BADO WASHIKILIWA NA TAKUKURU, KABURU NA AVEVA WA SIMBA NAO WAHOJIWA


RAIS wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Katibu Mkuu wake, Celestine Mwesigwa, wanashikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).

Viongozi hao wawili walikamatwa juzi kwa tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi, yakihusisha ubadhirifu wa mamilioni ya shirikisho hilo.

Malinzi na Mwesigwa hadi leo hii asubuhi bado walikuwa wakishikiliwa na taasisi hiyo na huenda Malinzi akashindwa kuhudhuria usaili wa wagombea wa nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu wa TFF.

TAKUKURU haikuwa tayari kusema lolote jana kuhusu kuwashikilia viongozi hao wawili na lini itawaachia.

Wakati huo huo, Rais wa klabu ya Simba, Evans  Aveva na makamu wake, Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ nao wanashikiliwa na TAKUKURU kwa ajili ya uchunguzi juu ya tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu kutokana na mchezaji Emmanuel Okwi.

Habari za uhakika kutoka kwa taasisi hiyo zimeeleza kuwa, viongozi hao wakuu wa klabu hiyo walikamatwa jana kwa nyakati tofauti kwa ajili ya mahojiano juu ya tuhuma hizo.

Kwa mujibu wa habari hizo, imedaiwa kuwa kulifanyika udanganyifu katika mauzo ya Okwi kwenda klabu ya Esperance ya Tunisia.

Imeelezwa kuwa Dola 300,000, ambazo ni zaidi ya sh. milioni 600, zilizotajwa kuwa Simba ililipwa kutokana na mauzo ya mchezaji huyo, sicho ilicholipwa.

NGOMA AKATA MZIZI WA FITINA, AONGEZA MKATABA WA MIAKA MIWILI YANGA



MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Zimbabwe, Donald Ngoma ametia saini mkataba mpya wa miaka miwili wa kuendelea kuichezea klabu ya Yanga.

Ngoma alirejea nchini mwanzoni mwa wiki hii huku kukiwa na taarifa kwamba, amejiunga na klabu ya Polokwane City ya Afrika Kusini kwa mkataba wa miaka mitatu.

Mwenyekiti wa Kamati ya usajili ya Yanga Hussein Nyika amethibitisha kumsaini mshambuliaji wa Zimbabwe Donald Ngoma kwa mkataba wa miaka miwili.

“Ngoma tumeshamsaini leo kwa mkataba wa miaka miwili kwa hiyo ataendelea kuitumikia Yanga kwa misimu miwili ijayo akiwa ni mchezaji halali wa Yanga.”

“Mashabiki wa Yanga waelewe kwamba, Ngoma bado yupo Yanga.”

Kabla ya Yanga kukata mzizi wa fitna kwa kumuongeza mkataba Ngoma, kulikuwa habari kwamba mchezaji huyo raia wa Zimbabwe huenda akatimkia Simba kwa ajili ya msimu ujao.

Ngoma aliwasili jana usiku na kupokewa na watu wa Yanga kabla ya kusaini mkataba mpya na mabingwa wa Tanzania leo Juni 29, 2017.

OKWI ATUA TENA MSIMBAZI




MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi ametia saini mkataba wa kuichezea klabu ya Simba kwa miaka miwili.

Okwi ametia saini mkataba huo mbele ya Makamu wa Rais wa Simba, Godfrey Nyange 'Kaburu'.

Baada ya kutia saini mkataba huo, Okwi alitambulishwa kwa waandishi wa habari mbele ya mfadhili wa klabu hiyo, Mohammed Dewji.

Akizungumza wakati wa utambulisho huo, Dewji alisema usajili wa Okwi ni zawadi ya sikukuu ya Idd el Fitr kwake kwa mashabiki wa Simba.

Kwa upande wake, Okwi aliwaahidi furaha mashabiki wa Simba kwa kuwarejeshea mataji ambayo iliyapoteza kwa miaka minne mfululizo.

Sunday, June 25, 2017

NYAMLANI AJITOA KUWANIA URAIS TFF



MAKAMU wa Rais wa zamani wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Athumani Nyamlani amejitoa kwenye kinyang’anyiro cha kuwania urais wa shirikisho hilo unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu.
Taarifa ya Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas imesema kwamba Nyamlani amewasilisha barua leo Jumapili Juni 25, mwaka huu ikiwa ni siku moja tu tangu Kamati ya Uchaguzi ipitishe jina lake kuwa miongoni mwa wagombea 10 wanaowania nafasi hiyo ya urais. Sababu aliyoeleza ni masuala binafsi.
Kwa msingi huo, wagombea wanaobaki kwenye kinyang’anyiro na kuhitajika kufika kwenye usaili kuanzia Juni 29, mwaka huu ni tisa wakiongozwa na Rais wa sasa, Jamal Malinzi anayetetea nafasi.

MO FLAVOUR, MSANII ALIYEPANIA KUITANGAZA TANZANIA KIMATAIFA



Na Mwandishi Wetu
KWA umri, msanii Mohamed Ngwenje, maarufu kwa jina la Mo Flavour, bado ni mdogo. Ndio kwanza amefikisha umri  wa miaka 19, ikiwa ni miaka michache baada ya kumaliza elimu ya sekondari katika shule ya Uwanja wa Taifa, iliyoko mkoani Morogoro.
Pamoja na umri wake huo mdogo na pia kuwa na miaka michache tangu alipojitosa katika fani ya muziki wa kizazi kipya, msanii huyo ameshafanya mambo makubwa mawili.
Kwanza amesharekodi nyimbo mbili, Usibeti aliouimba peke yake na Kusudi, ambao ameuimba kwa kushirikiana na wanamuziki nyota wawili nchini, Jose Mara na Khalid Chuma ‘Chokoraa’.
Wimbo wake wa Usibeti ndio uliomtambulisha katika anga za muziki huo wa kizazi kipya na ndio uliomwezesha kukutana na Jose Mara na Chokoraa na hatimaye kukubali kurekodi naye wimbo wa Kusudi.
Tayari Mo Flavour ameshaurekodi wimbo wa Usibeti kwenye video na audio na kwa sasa anafanya mipango ya kurekodi video ya wimbo wa Kusudi, baada ya kukamilisha kazi ya kurekodi audio.
Mo Flavour amerekodi nyimbo hizo kwenye studio za Moro Town Records ya Morogoro na Amoroso Sound ya Dar es Salaam, ambayo ilitumika kuchanganya ala za muziki kitaalamu zaidi.
Kwa mujibu wa msanii huyo chipukizi, alifanikiwa kurekodi nyimbo hizo kwa udhamini wa baba yake mzazi, Ngwenje Mohamed, ambaye pia amekuwa akimtumia kama meneja wake.
“Kwa sasa baba ndiye kila kitu kwangu katika masuala ya muziki, lakini lengo langu kubwa huko mbele ni kuwa na meneja wa uhakika kwa ajili ya kusimamia kazi zangu,”alisema Mo Flavour, alipozungumza na Uhuru, hivi karibuni mjini Dar es Salaam.
Msanii huyo, ambaye kwa sasa anachukua masomo ya kompyuta katika Chuo cha Royal, kilichoko Ubungo, Dar es Salaam, alisema anamshukuru Mungu kwamba, nyimbo zake zote mbili zimepokelewa vizuri na mashabiki wa muziki wa kizazi kipya.
Alisema kupokelewa vizuri kwa nyimbo hizo, kulijidhihiridha wakati wa utambulisho wa kibao chake cha kwanza cha Usibeti, alioufanya mwaka jana, kwenye ukumbi wa Jahazi Garden, mjini Morogoro.
Kwa mujibu wa Mo Flavour, alifanya onyesho hilo la uzinduzi kwa udhamini wa baba yake na kuongeza kuwa, lilihudhuriwa na mashabiki lukuki.
“Hata mapato niliyoyapata yalikuwa mazuri na ndiyo yaliyoniwezesha kupata fedha za kurekodi wimbo wangu uliofuata wa Kusudi,”alisema Mo Flavour.
Mbali na mafanikio hayo, alisema amekuwa akipata mialiko mingi ya kufanya maonyesho mbalimbali ya muziki huo kwa kushirikiana na baadhi ya wasanii maarufu nchini.
“Jambo la kufurahisha ni kwamba, nimeanza kupokea mialiko kutoka hata katika nchi jirani za Uganda na Kenya. Hii inadhihirisha kwamba, kazi zangu zinakubalika,”alisema.
Akizungumzia hali ya muziki huo nchini, Mo Flavour alisema ni nzuri na ya kuridhisha kutokana na mafanikio yaliyofikiwa na wasanii wengi wa fani hiyo.
Hata hivyo, alikiri kuwa kikwazo kikubwa kwa wasanii wanaochipukia ni kukosa promosheni kwa vile mapromota wanapenda zaidi kuwasaidia wasanii waliokwishapata umaarufu, badala ya wale wanaochipukia.
“Unaweza kutunga nyimbo nzuri na kali, ikapendwa na mashabiki, lakini ikakosa mtu wa kuitangaza. Hali hii imekuwa ikisababisha wasanii wengi wanaochipukia kukata tamaa mapema,”alisema.
Msanii huyo amesema anamshukuru Mungu kwa kupata uungwaji mkono wa kiwango kikubwa kila alipotembelea vituo mbalimbali vya redio na televisheni nchini. Alisema hali hiyo imekuwa ikimtia moyo na kumfanya ajitume zaidi.
“Japokuwa kumekuwa na malalamiko ya watangazaji wa redio na televisheni kubania kazi za wasanii, kwangu mimi hali ni tofauti. Kila ninapopeleka kazi zangu kwenye vituo vya redio na televisheni, zimekuwa zikikubalika. Sikuwahi kuombwa rushwa,”alisema.
Msanii huyo pia amesema anaunga mkono uwepo wa sheria ya hatimiliki nchini, ambayo inamwezesha msanii kulipwa kila kazi yake inapotumika kwenye vituo vya redio na televisheni.
Amesema kazi ya muziki ni biashara, vivyo hivyo vituo vya redio na televisheni navyo vimekuwa vikifanya biashara, hivyo vinapotumia kazi za wasanii, havina budi kuwalipa.
Mo Flavour amesema binafsi anavutiwa na wasanii wote wa kizazi kipya nchini kwa kuwa kila mmoja anajitahidi kufanya vizuri ili aweze kupata mafanikio.
Ameyataja malengo yake katika siku zijazo kuwa ni pamoja na kuitangaza Tanzania kimataifa kupitia muziki huo na pia kuwa mwanamuziki wa kimataifa.
Amewataka wasanii wa muziki huo wawe makini katika kazi yao, hasa wanapobahatika kupata udhamini kutoka kwenye kampuni na watu binafsi.
“Nawashauri wasanii wenzangu unapopata msaada wa udhamini, jitume. Huwezi kuendelea kusaidiwa kama hufanyi jambo la maana,”alisema.
Pia, aliwataka wasanii wa muziki huo kuacha tabia ya kujikweza na kujiona wapo matawi ya juu pale wanapoanza kupata mafanikio. Alisema kufanya hivyo kunawakera mashabiki na kutasababisha waporomoke mapema kimuziki.
0000000


















TAIFA STARS, MALAWI KAZI IPO LEO KOMBE LA COSAFA


Kikosi cha wachezaji 22 wa timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, kimesafiri na kufika salama nchini Afrika Kusini kikitokea Dar es Salaam, Tanzania.

Timu hiyo iliyoondoka jana Alhamisi Juni 22, 2017 kwenda Afrika Kusini kwa ndege ya Shirika la Ndege la Rwanda, itakuwa huko kwa ajili ya michuano ya kuwania Kombe la Castle Cosafa.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti, itaanza kampeni za kucheza hatua ya Robo fainali kwa kucheza na Malawi Jumapili, Juni 25, mwaka huu katika michuano hiyo iliyoandaliwa na Baraza la Mpira wa Miguu la nchi za Kusini mwa Afrika (Cosafa).

Tanzania si mwanachama wa Cosafa, lakini imealikwa katika mashindano hayo na imepangwa kundi A na timu za Mauritius, Malawi na Angola wakati Kundi B ni Msumbiji, Shelisheli, Madagascar na Zimbabwe. Kinara wa kila kundi atakwenda moja kwa moja hatua ya robo fainali.

Timu za Botswana, Zambia na Afrika Kusini kadhalika Namibia, Lesotho na Swaziland tayari zimepangwa hatua ya robo fainali hivyo zinasubiri vinara wawili kutoka makundi ya A na B kuungana nazo kucheza robo fainali.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Shabani Mayanga, amesema kwamba anaichukulia michuano hiyo kwa umakini na uzito mkubwa kwa wachezaji kuzidi kupata uzoefu wa mechi nyingi za kimataifa kwa mwaka.

Kadhalika, kiufundi Mayanga anachukulia michuano hiyo kama sehemu ya maandalizi makubwa ya mchezo dhidi ya Rwanda wa kuwania kucheza nafasi ya kushiriki fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ligi za ndani - CHAN.

Mchezo huo wa kwanza utafanyika Julai 15, mwaka huu kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, jijini Mwanza.

Kikosi cha Taifa Stars kilichopo Afrika Kusini kinaundwa na makipa Aishi Salum Manula  (Azam FC), Benno David Kakolanya  (Young Africans SC) na Said Mohammed Said (Mtibwa Sugar FC).

Walinzi wa pembeni upande wa kulia ni Shomari Salum Kapombe    (Azam FC) na Hassan Hamis Ramadhan ‘Kessy’ (Young Africans SC) wakati upande wa kushoto wapo Gadiel Michael (Azam FC) na Hamim Abdulkarim (Toto Africans FC).

Walinzi wa kati ni Erasto Nyoni  (Azam FC), Salim Hassan Abdallah (Mtibwa Sugar), Abdi Hassan Banda (Simba SC) na Nurdin Chona (Tanzania Prisons) wakati viungo wa kuzuia kuwa ni Himid Mao Mkami (Azam FC) na Salmin Hoza wa Mbao FC.

Kadhalika wako viungo wa kushambulia ambao ni Mzamiru Yassin Selembe (Simba), Simon Happygod Msuva (Young Africans SC), Raphael Daudi (Mbeya City) na Shizza Ramadhani Kichuya (Simba SC).

Katika safu ya ushambuliaji wamo Thomas Emmanuel Ulimwengu (AFC Eskilstuna – Sweden), Mbaraka Abeid Yusufu (Kagera Sugar), Stamili Mbonde, Elius Maguli (Dhofar SC) na Shabani Idd Chilunda (Azam FC).

WANAWAKE WAJITOKEZA UCHAGUZI TWFA, WAPITISHWA

Wanawake wamejitokeza kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika Chama cha Mpira wa Miguu Wanawake (TWFA) katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Julai 8, mwaka huu.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, Msomi Wakili George Mushumba leo Juni 23, aliongoza kikao cha Kamati ya Uchaguzi kupitia majina ya wagombea walioomba kugombea nafasi mbalimbali.

Mara baada ya kikao hicho, amewataja wanaowania nafasi mbalimbali kwenye mabano kuwa ni Amina Karuma (Nafasi ya Uenyekiti); Rose Kissiwa (Makamu Mwenyekiti); Somoe Ng’itu (Katibu) na Theresia Mung’ong’o (Katibu Msaidizi ).

Nafasi ya Mweka Hazina, kwa mujibu wa Mushumba inawaniwa na Hilda Masanche ilihali nafasi ya Ujumbe wa Mkutano Mkuu TFF, inawaniwa na Salma Wajesso na Zena Chande huku Ujumbe wa Kamati ya Utendaji TWFA waliopitishwa ni Triphonia Temba, Jasmine Badar, Chichi Mwidege na Mwamvita Kiyogomo.

Musumba ametangaza majina hayo ya wagombea waliostahili au waliotimiza taratibu za uchaguzi kwa mujibu wa katiba na kanuni za uchaguzi za TWFA.

Kinachofuata kwa sasa ni kwamba Juni 26 na 27, 2017- Kupokea pingamizi kati ya saa 4:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni katika ofisi za TFF.
Juni 28, 2017- Kamati ya Uchaguzi kupitia pingamizi kama zimewasilishwa.
Juni 29, 2017-  Kamati kutoa majumuisho ya pingamizi kama ziliwasilishwa na wadau.
Juni 30, 2017-  Usaili kwa wagombea waliotangazwa.
Julai 01, 2017- Kutangaza majina ya wagombea waliopitishwa
Julai 02, 2017-Kamati kupokea rufaa
Julai 03, 2017-  Kamati kupitia rufaa kama zimewasilishwa.
Julai 04, 2017   Kamati kutangaza orodha ya mwisho ya wagombea.
Julai 04 hadi 07, 2017 - Wagombea kufanya kampeni kwa kuzingatia maadili.
Julai 08, 2017- Uchaguzi Mkuu wa TWFA

Thursday, June 22, 2017

KOZI YA WAAMUZI YASOGEZWA MBELE

Kozi ya waamuzi wa mpira wa miguu, iliyolenga kuwainua  madaraja kutoka madaraja waliyonayo sasa hadi ngazi moja juu, imesogezwa mbele kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Waamuzi ya TFF, Saloum Chama.
 
Chama amesema kwamba kozi hiyo iliyopangwa kufanyika kuanzia Juni 29, mwaka huu itafanyika hapo baadaye katika tarehe itakayopangwa, lakini itakuwa ni kabla ya  Uchaguzi Mkuu wa TFF.
 
“Watu wasiende kuripoti hiyo Juni 29, mwaka huu kama tulivyotangaza. Tumesogeza mbele kidogo kozi hii. Tarehe mpya itatangazwa hapo baadaye,” amesema Chama ambaye alitaja vituo vilivyopangwa kuwa ni Mwanza, Ruvuma na Dodoma.

UCHAGUZI RUREFA KUFANYIKA JULAI 5, 2 017


Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), imetangaza kuwa Uchaguzi Mkuu wa Chama cha Soka Mkoa wa Rukwa (RUREFA), utafanyika Agosti 05, mwaka huu mjini Sumbawanga.

“Napenda kuwatangazia wadau wote wa RUREFA kuwa mchakato wa uchaguzi utaendelea kuanzia pale ulipokomea,” alisema Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi wa TFF, Wakili Revocatus Kuuli mara baada ya kikao cha Kamati hiyo, kilichoketi Juni 10, mwaka huu.

Wakili Kuuli amesema uchaguzi utaendeshwa na Kamati ya Uchaguzi ya RUREFA, kwa kusimamiwa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF kama ilivyoanishwa kwenye taarifa ya awali.

Sasa kinachofuata ni kipindi cha kupokea na kuweka pingamizi kwa wagombea ambapo zoezi hilo litafanyika Julai 4 na 5, 2017 wakati Julai 6 na 7, mwaka huu itakuwa ni kupitia pingamizi zote na kufanya usaili wa wagombea.

Kwa mujibu wa ratiba iliyotangazwa, Julai 8, mwaka huu itakuwa ni hatua ya kutangaza na kubandika kwenye mbao za matangazo matokeo ya awali ya usaili ilihali Julai 9 na 10, mwaka huu Sekretariati kuwasilisha masuala ya kimaadili kwenye kamati ya Maadili.


Kuanzia Julai 11 hadi 13, mwaka huu itakuwa ni kipindi cha kupokea na kusikiliza na kutolea maamuzi masuala ya maadili wakati Julai 14 na 15, mwaka huu ni kutangaza matokeo ya uamuzi wa Kamati ya Maadili huku Julai 16 na 17, itakuwa ni kipindi cha kukata Rufaa kwa maamuzi ya masuala ya kimaadili kwenye kamati ya rufaa ya maadili ya TFF.

Julai 18 na 19, mwaka huu itakuwa ni kipindi cha kusikiliza rufaa za kimaadili wakati Julai 20 na 21 ni kutoa uamuzi wa Rufaa huku Julai 22 na 23, ni kipindi cha kukata rufaa dhidi ya Kamati ya Uchaguzi kwenye kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF.

Julai 24 hadi 26, ni kipindi cha kusikilizwa rufaa kazi itakayofanywa na Kamati ya rufaa ya Uchaguzi ya TFF ilihali Julai 27 na 28, ni kwa wagombea na kamati ya uchaguzi kujulishwa maamuzi ya Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF.

Julai 29 na 30, mwaka huu ni kuchapisha orodha ya mwisho ya wagombea na kutangazwa na kubandikwa kwenye mbao za matangazo wakati kipindi cha kampeni kwa wagombea kitakuwa ni kati ya Julai 31 hadi Agosti 4, mwaka huu. Uchaguzi Mkuu wa RUREFA utakuwa Agosti 5, mwaka huu.

Hatua za awali zilizofanyika, kabla ya kusimamishwa uchaguzi kutangaza mchakato wa Uchaguzi wa TFF nafasi zinazogombewa na kubandika kwenye mbao za matangazo; kuchukua na kurudisha fomu za kuomba uongozi; hatua ya mchujo na kuchapisha na kubandika kwenye mbao za matangazo orodha ya awali ya wagombea.

TAIFA STARS YAENDA AFRIKA KUSINI


Kikosi cha wachezaji 22 wa timu ya Tanzania ‘Taifa Stars’, kinaondoka leo Alhamisi Juni 22, 2017 kwenda Afrika Kusini katika michuano ya kuwania Kombe la Castle Cosafa.

Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti, ilikuwa kambini Hoteli ya Urban Rose, iliyoko Mtaa wa Jamhuri katikati ya jiji la Dar es Salaam, tangu Jumapili Juni 18, mwaka huu.

Taifa Stars imeandaliwa kwa michuano hiyo iliyoandaliwa na Baraza la Mpira wa Miguu la nchi za Kusini mwa Afrika. Tanzania si mwanachama wa Cosafa, lakini imealikwa katika mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza Juni 25, mwaka huu.

Taifa Stars imepangwa kundi A na timu za Mauritius, Malawi na Angola wakati Kundi B ni Msumbiji, Shelisheli, Madagascar na Zimbabwe. Timu za Botswana, Zambia na Afrika Kusini kadhalika Namibia, Lesotho na Swaziland zitakuwa na mechi maalumu (play off) ili kuingia robo fainali.

Kwa mujibu wa Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Salum Mayanga, kikosi kinachoondoka leo ni makipa Aishi Salum Manula  (Azam FC), Benno David Kakolanya  (Young Africans SC) na Said Mohammed Said (Mtibwa Sugar FC).

Walinzi wa pembeni upande wa kulia ni Shomari Salum Kapombe    (Azam FC) na Hassan Hamis Ramadhan ‘Kessy’ (Young Africans SC) wakati upande wa kushoto wapo Gadiel Michael (Azam FC) na Amim Abdulkarim (Toto Africans FC).

Walinzi wa kati ni Erasto Nyoni  (Azam FC), Salim Hassan Abdallah (Mtibwa Sugar), Abdi Banda (Simba SC) na Nurdin Chona (Tanzania Prisons) wakati viungo wa kuzuia kuwa ni Himid Mao (Azam FC) na Salmin Hoza wa Mbao FC.

Kadhalika wako viungo wa kushambulia ambao ni Mzamiru Yassin Selembe (Simba), Simon Happygod Msuva (Young Africans SC), Raphael Daudi (Mbeya City) na Shizza Ramadhani Kichuya (Simba SC).

Katika safu ya ushambuliaji wamo Thomas Emmanuel Ulimwengu (AFC Eskilstuna – Sweden), Mbaraka Abeid Yusufu (Kagera Sugar), Stamili Mbonde, Elius Maguli (Dhofar SC) na Shabani Idd Chilunda (Azam FC).

SERIKALI YAUNGA MKONO VIONGOZI WA TFF KUTOKUWA NA KOFIA MBILI



Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison G. Mwakyembe amempongeza Mwenyekiti wa Baraza la Michezo la Taifa (BMT), Dionis Malinzi, kwa hatua kadhaa ambazo baraza lake limeanza kuchukua katika kusimamia michezo nchini, likiwemo zuio kwa viongozi kuwa na kofia mbili kwenye mchezo mmoja.

Katika salamu alizomtumia kiongozi huyo wa BMT jana jioni, Dk. Mwakyembe amesema hatua hizo zimeonesha uhai, uhalali na hitaji la uwepo wa BMT kwa maendeleo ya michezo nchini.

Dk. Mwakyembe amesema Wizara haitarajii tena kuona kiongozi katika mchezo wowote ule nchini kuwa na kofia mbili kinyume na sheria na kanuni zilizopo, huku BMT ikiangalia pembeni na kuinyamazia hali hiyo.

Waziri Mwakyembe vilevile amesema Wizara haitarajii kuona chombo chochote cha michezo nchini kikikiuka Kanuni na Sheria za nchi bila kuchukuliwa hatua stahiki kwa kisingizio kuwa kinawajibika kwa vyombo vya kimataifa, kwani kisingizio hicho ni batili kikatiba na kisheria hivyo hakiwazuii BMT kutekeleza wajibu wao kwa mujibu wa Sheria za nchi.

Aidha amewapa pole BMT kwa kuondokewa na mwanamichezo maarufu nchini Ally Mohammed, a.k.a. Ally Yanga, aliyefariki dunia jana (Jumanne) kwa ajali ya gari wilayani Mpwapwa.

“Tumepoteza kifaa muhimu katika kuhamasisha michezo nchini na nifikishieni salamu zangu za rambirambi kwa ndugu, jamaa, marafiki wa marehemu na wanamichezo wote nchini”, Dk. Mwakyembe amesema na kuwatakia BMT mafanikio katika utekelezaji wa majukumu yao.

Imetolewa na:
Genofeva Matemu
Kaimu Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini,
Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo
21/06/2017

YANGA YATANGAZA RASMI KUACHANA NA NIYONZIMA



Taarifa rasmi kutoka klabu ya Yanga ni kwamba, imeamua kuachana na kiungo wake wa kimataifa wa Rwanda Haruna Niyonzima baada ya kushindwa kufikia makubalino kuhusu kuongeza mkataba mpya wa kuendelea kubaki Yanga.

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa amesema, Yanga imeamua kuachana na Niyonzima baada ya pande hizo mbili kushindwa kufikia makubaliano juu ya kuongeza mkataba mpya ambao ungemfanya Niyonzima aendelee kusalia kwa mabingwa hao wa VPL.

“Tumekuwa na changamoto nyingi haswa katika kipindi hiki cha usajili kuna taarifa mbalimbali zimekuwa zikitoka kuhusiana na mchezaji ambaye alikuwa ni nahodha wetu msaidizi Haruna Niyonzima, ni kweli mkataba wake unakaribia kukamilika na sisi kama viongozi tumefanya jitihada za kukutana naye kujaribu kuongeza mkataba kwa kipindi kijacho kwa sababu bado tulikuwa na nia nae.”

“Tumekuwa tukikaa na kamati pamoja na viongozi kwa kipindi kirefu lakini kumetokea kutoelewa kutokana na matakwa yake yaliyokuwa yamejitokeza kwa hiyo klabu inasema wazi kwamba klabu hakuwa na uwezo wa kile ambacho kilikuwa kinatakiwa na mchezaji kwa hiyo imeshindikana kulingana na hali ya klabu ilivyo.”

“Muda ukifika tutamruhusu na kumtakia kila la heri kule anakokwenda kwa faida yake mwenyewe na familia yake, kweli sisi tulikuwa na nia yake na tulizungumza nae lakini hatukufikia makubaliano  na sisi kwa maslahi ya klabu tumeamua tumruhusu aende kule ambako anaweza kupata maslahi mazuri.”

Kwa mujibu wa Mkwasa, Niyonzima alikuwa akihitaji pesa ndefu ili asaini mkataba mpya kitu ambacho Yanga walishindwa kufikia makubaliano nae na kuamua kumruhusu aende sehemu ambako atapata dau hilo.

“Kwa tamaduni zetu huwa hatusemi ni kiasi gani lakini nafikiri ni kiasi kikubwa siwezi kukitaja kwa umma kwa hiyo kwa maslahi ya klabu tumeona ni bora tufanye utaratibu mwingine kwa sababu tunaweza kufanya usajili mwingine kuliko ambavyo tungeweza kutoa kiasi hicho kwa mtu mmoja.”

Niyonzima amekuwa akihusishwa kujiunga na klabu ya Simba ambayo imekuwa ikimuwinda kwa muda lakini mara kadhaa amekuwa akikanusha taarifa hizo na kudai yeye bado ana mkataba na Yanga.

Tuesday, June 20, 2017

ALLY YANGA AFARIKI KWA AJALI DODOMA


Kamanda wa polisi Mkoa wa Dodoma, Lazaro Mambosasa amethibitisha kifo cha aliyekuwa shabiki maarufu wa klabu ya soka ya Yanga Ally Yanga kilichotokea leo katika ajali ya gari aina ya Rav4 eneo la Chipogolo wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma.

Ally Yanga ambaye pia ni mkereketwa wa Mwenge wa Uhuru alikutwa na mauti akiwa katika gari la kampuni ya Faidika ambalo lilikuwa kwenye shughuli zake za promosheni na SIO KWAMBA alikuwa kwenye msafara wa Mwenge kama inavyoenezwa.

Ally aliyezaliwa mkoani Shinyanga Machi 1, mwaka 1984 katika familia ya watoto sita, kabla ya umauti wake inafahamika alikuwa anaishi Yombo Vituka, Dar es Salaam.

Lakini tangu baada ya uchaguzi Mkuu Novemba 2015, Ally Yanga ameadimika viwanja vya soka kutokana na kujikita zaidi kwenye shughuli za Chama cha Mapinduzi CCM.

BANDA AMALIZANA NA SIMBA, KUMWAGA WINO MUDA WOWOTE


Beki wa timu ya Taifa na klabu ya Simba Abdi Hassan Banda ameweka wazi msimamo wake wa kuendelea kuitumikia timu yake hiyo kwa mkataba wa miaka wa miaka miwili ila amewataka kuweka kipengele cha kumuachia iwapo atapata timu nyingine nje.

Ameyasema hayo wakati wa mazoezi ya timu ya Taifa kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya COASAFA inayotarajiwa kuanza Juni 25 nchini Afrika Kusini. Banda amekubali kusaini kandarasi na timu yake ya Simba huku akiwa amepatiwa dau la maana ambalo limeweza kumshawishi kuendelea kusalia kwa wana msimbazi hao.

Taifa Stars inayojiandaa na michuano ya COSAFA Castle nchini Afrika Kusini baadaye mwezi huu, Banda amesema kwamba wakati wowote, Meneja wake Abdul Bosnia atafika Dar es Salaam ili wasaini mkataba huo mpya na Simba.

“ Mkataba wangu na klabu ya Simba umesalia siku tano, lakini tumeshafikia makubaliano na nitaendelea nao baada ya kusaini mkataba huo inaweza kuwa  kabla sijaenda Afrika Kusini au baada ya kurejea kutoka huko,"amesema Banda.

Ameweka wazi kuwa,  mazungumzo baina yake na uongozi wa Simba umekuwa mzuri na wenyewe wanajua makubaliano yao ili aweze kuongeza mkataba na kuendelea kuitumikia klabu hiyo na zaidi anamsubiri meneja wake aje kumalizana nao.

Banda yumo kwenye kikosi cha Taifa Stars, kinachotarajiwa kushiriki michuano ya Kombe la Mataifa ya Kusini mwa Afrika (COSAFA) Castle nchini Afrika Kusini kuanzia Juni 25, mwaka huu.

Taifa Stars iliyoweka kambi hoteli ya Urban Rose iliyopo iliyopo eneo la Kisutu, huku ikifanya mazoei Uwanja wa JMK Youth Centre, inatarajiwa kuondoka nchini Juni 22 kwenda Afrika Kusini kushiriki michuano ya COSAFA kama wa waalikwa kwa mwaka wa pili mfululizo na mara ya tatu kwa ujumla kihistoria.

Tanzania imepangwa kundi A pamoja na Mauritius, Malawi na Angola wakati Kundi B lina timu za Msumbiji, Shelisheli, Madagascar na Zimbabwe – na Botswana, Zambia, Namibia, Lesotho na Swaziland na wenyeji, Afrika Kusini zitacheza mechi maalumu za mchujo kuwania kuingia robo faina.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

NGULI WA TIMU ZA TAIFA ZA WANAWAKE DUNIANI KUCHEZA MECHI YA KIRAFIKI KATIKA KRETA YA MLIMA KILIMANJARO






BMT YABARIKI UCHAGUZI TFF, LATOA MAAGIZO


Baraza la Michezo Tanzania (BMT), limebariki Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) likisema: “Tunaitakia TFF uchaguzi mwema wenye amani, upendo na utulivu.”

Pamoja na baraka hizo, Baraza limeiagiza TFF kuwaelekeza wagombea wote kuzipitia sheria za Baraza la Michezo, Kanuni za Baraza na kanuni za Usajili, hususani kanuni ya 8 (1) na (2).

Kanuni hiyo ya 8 (1) na (2), inaagiza kuwa endapo wagombea wote watakaoshinda nafasi wanazowania kwa sasa ndani ya TFF, hawana budi kuachia nafasi mojawapo katika uongozi wa mpira kwa miguu katika ngazi ya wilaya au mkoa aliyoshinda awali.
 
BMT imetoa agizo hilo ikiwa ni kukumbushana juu ya utii wa sheria na kuepuka kushika nyadhifa mbili kwa wakati mmoja.

Katika barua yake iliyoandikwa Juni 19, mwaka huu na kusainiwa na Katibu Mkuu wa BMT, Mohammed Kiganja, Baraza hilo limesema: “Uchaguzi huu usivuruge amani iliyopo nchini. Wagombea wakumbuke kuwa kuna maisha baada ya uchaguzi.”

Baraza limesisitiza kuwepo na haki katika mchakato mzima kuelekea kwenye uchaguzi.

Uchaguzi na mchakato wake uwe huru na amani na usiwe ni kichocheo cha uvunjifu wa amani.


Baada ya viongozi kupatikana, watakula kiapo cha utii, na kujaza fomu Namba 5 ya BMT ya utekelezaji majukumu yao kama Kanuni ya 8 (4) inavyoeleza.


Kadhalika, mara baada ya uchaguzi, Baraza limeagiza kuhusisha baadhi ya vifungu vya sheria ya Baraza ili viendane na katiba za TFF na wadau pamoja na kanuni zao.

74 WACHUKUA FOMU, KUREJESHA TFF



Wanafamilia 74 wa mpira wa miguu, wamechukua na kurejesha fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) katika uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu.
 
Hadi zoezi hilo linafungwa leo Juni 20, 2017 saa 10.00 jioni wagombea wote wamerejesha ambako kwenye nafasi ya urais, jumla ya wagombea 10 walijitokeza kuomba nafasi hiyo wakati kwenye makamu rais wamejitokeza sita.

Wadau 58 wamejitokeza kuwania nafasi za ujumbe wa kamati ya utendaji katika Katika Kanda mbalimbali. Zoezi la kuchukua na kurejesha fomu kwa mujibu wa Kanuni ya 10, limefanyika kwa siku tano kuanzia Juni 16, 2017 hadi Juni 20, mwaka huu.

Siku ya kwanza ilipoanza tu, Jamal Malinzi alikuwa wa kwanza kuchukua fomu na kurejesha huku akifuatiwa na Imani Madega, Wallace Karia, Fredrick Masolwa, Athumani Nyamlani, Fredrick Mwakalebela, John Kijumbe, Shija Richard, Ally Mayay na Emmanuel Kimbe.


Waliojitokeza kuwania Makamu wa Rais na kurejesha fomu wako Mulamu Ng’hambi, Michael Wambura, Geofrey Nyange, Mtemi Ramadhani, Robert Selasela na Stephen
Mwakibolwa.

Wajumbe wa Kamati ya Utendaji kwa kufuata Kanda 13 ni kama ifuatavyo:

Kanda Na. 1 Mikoa ya Kagera na Geita;

    Soloum Chama
    Kaliro Samson
    Leopold Mukebezi
    Abdallah Mussa

Kanda Na. 2 Mikoa ya Mara na Mwanza;

    Vedastus Lufano
    Ephraim Majinge
    Samwel Daniel
    Aaron Nyanda

Kanda Na. 3 Mikoa ya Shinyanga na Simiyu;

    Benista Rugora
    Mbasha Matutu
    Stanslaus Nyongo

Kanda Na. 4 Mikoa ya Arusha na Manyara;

    Omari Walii
    Sarah Chao
    Peter Temu

Kanda Na. 5 Mikoa ya Kigoma na Tabora;

    John Kadutu
    Issa Bukuku
    Abubakar Zebo
    Francis Michael

Kanda Na. 6 Mikoa ya Katavi na Rukwa;

    Kenneth Pesambili
    Baraka Mazengo

Kanda Na. 7 Mikoa ya Mbeya, Songwe na Iringa;

    Elias Mwanjala
    Cyprian Kuyava
    Erick Ambakisye
    Abousuphyan Silliah

Kanda Na. 8 Mikoa ya Njombe na Ruvuma;

    James Mhagama
    Golden Sanga
    Vicent Majili
    Yono Kevela

Kanda Na. 9 Lindi na Mtwara;

    Athuman Kambi
    Dunstan Mkundi

Kanda Na. 10 Mikoa ya Dodoma na Singida;

    Hussein Mwamba
    Mohamed Aden
    Musa Sima
    Stewart Masima
    Ally Suru
    George Benedict

Kanda Na. 11 Mikoa ya Pwani na Morogoro;

    Charles Mwakambaya
    Gabriel Makwawe
    Francis Ndulane
    Hassan Othman ‘Hassanol’

Kanda ya 12. Mikoa ya Kilimanjaro na Tanga
    Khalid Mohamed
    Goodluck Moshi
    Thabit Kandoro

Kanda Na. 13 Mkoa wa Dar es Salaam

    Emmanuel Ashery
    Ayoub Nyenzi
    Saleh Alawi
    Shaffih Dauda
    Abdul Sauko
    Peter Mhinzi
    Ally Kamtande
    Said Tully
    Mussa Kisoky
    Lameck Nyambaya
    Ramadhani Nassib
    Aziz Khalfan
    Jamhuri Kihwelo
    Saad Kawemba
    Bakari Malima

Kwa siku tatu, kuanzia kesho Juni 21 hadi 23, mwaka huu kwa mujibu wa kanuni ya 11.1 ya Uchaguzi wa TFF, Kamati ya Uchaguzi itaanza mchujo wa awali kwa wote waliojitokeza kuwania nafasi mbalimbali kama inavyojionesha hapo juu.

Sunday, June 18, 2017

SINGIDA UNITED YAMNASA NYOTA WA KIMATAIFA WA RWANDA


Timu ya Singida United imekamilisha usajili wa mshambuliaji wa Rwanda ambaye alikuwa anacheza timu ya Polisi,Danny Usengimana na kuwa mchezaji wa sita wa kigeni kusajiliwa na matajiri hao.

Mshambuliaji huyu anayetabiliwa kuwa nitishio katika kufumani nyavu ukanda wa Afrika Mashariki na Kati ameingia kandarasi ya miaka miwili na kikosi cha Kocha Mkuu wa zamani wa Mabingwa Ligi Kuu ya Tanzania bara Yanga ,Hans Van Der Pluijm.

Timu ya Singida United ni timu tatu zilizopanda kushiriki Michuano ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania bara na nyingine ni Lipuli pamoja na Njombe Mji.

HATIMAYE MKUDE AMWAGA WINO SIMBA


Hatimaye Nahodha wa klabu ya Simba, Jonas Mkude amezima ndoto za Yanga baada ya kuongeza mkataba na klabu yake hiyo wa miaka miwili wa kukitumikia kikosi cha mabingwa wa Kombe la FA.

Kulikuwa na mvutano na timu yake kwa dau kubwa ambalo alilokuwa anataka huku kukienea tetezi kuwa mahasimu wao wakubwa Yanga walikuwa wanamhitaji hii baada ya mshambuliaji wao hatari Ibrahimu Ajibu kujiunga na Mabingwa hao wa kihistoria nchini Tanzania.

“Ameongeza mkataba wa miaka miwili, ilikuwa ni baada ya kukamilisha majadiliano ambayo yalikuwa yamefikia zaidi ya asilimia 99,” kilieleza chanzo.

VIGOGO WAZIDI KUJITOSA UCHAGUZI MKUU WA TFF


Uchaguzi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), umepangwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu mjini Dodoma.
Tayari wagombea wameanza kuchukua fomu na wamekuwa wakijitokeza kwa kasi kubwa.
Kinachoshangaza zaidi ni idadi kubwa ya wale wanaowania nafasi ya urais inayoshikiliwa na Jamal Malinzi.
Waliojitokeza ni watatu hadi sasa wakionyesha kwamba wanaitaka nafasi hiyo ili kufanya sahihi zaidi.
Wadau hao wamejitokeza kuchukua fimu hizo kwa kipindi cha siku mbili tu, yaani jana Ijumaa na leo Jumamosi katika ofisi za TTF, Karume jijini Dar es Salaam.
URAIS
Jamal Malinzi
Imani Madega
Wallace Karia
Fredrick Masolwa
MAKAMU RAIS
Mulamu Nghambi
Michael Wambura
Geofrey Nyange
WAJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI
Soloum Chama
Ephraim Majinge
Elias Mwanjala
Saleh Alawi
Kaliro Samson
Vedastus Lufano
Kenneth Pesambili
Mbasha Matutu
Samwel Daniel
Dunstan Mkundi
Athuman Kambi
Shaffi Dauda
Golden Sanga
Charles Mwakambaya
Benista Rugola.
Thabit Kandoro
Goodluck moshi
James Mhagama
Husen Mwamba
Sarah Chao
Isaa bukuku
Stewat Masima
Emmanuel Ashery
Abdul Sauko
Musa Sima
Stanslaus Nyongo
Ayoub Nyenzi
John Kadutu
Baraka Mazengo
Khalid Mohamed
Mohamed Aden
Cyprian Kuyava
Saleh Abdul
IMETOLEWA NA LEO
Alfred Lucas

Ofisa Habari TFF

Saturday, June 17, 2017

HANSPOPE AMPANDIA NDEGE OKWI NA KUNASA SAINI YAKE

HATIMAYE klabu ya Simba imekamilisha mipango ya kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Uganda, Emmanuel Okwi.
Simba imenasa saini ya mchezaji huyo baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili, Zacharia Hanspope kufunga safari kwenda Kampala, Uganda kukamilisha mazungumzo na nyota huyo.
Okwi ni miongoni mwa wachezaji wa zamani wa Simba walioiletea mafanikio makubwa klabu hiyo katika ligi kuu ya Tanzania na michuano ya kimataifa.
Hata hivyo, bado haijawekwa wazi kuhusu kiwango cha fedha alicholipwa mshambuliaji huyo ili arejee Simba.

MCHAKATO WA UCHAGUZI WA CHAMA CHA SOKA LA WANAWAKE TANZANIA (TWFA)


Kamati ya Uchaguzi ya Chama cha Mpira wa Miguu Wanawake (TWFA), leo Juni 16, 2017 imetangaza rasmi Uchaguzi wa chama hicho utakaofanyika Julai 8, mwaka huu.
Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi ya TWFA, George Mushumba amesema kwamba fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika chama hizo zitaanza kutolewa Juni 19, mwaka huu na kwamba mwisho wa kuchukua na kurudisha ni Juni 22, mwaka huu saa 10.00 jioni. Ratiba kamili kuelekea uchaguzi huo ni kama ifuatavyo:-
Juni 23, 2017- Kamati ya Uchaguzi kupitia majina ya wagombea walioomba kugombea nafasi mbalimbali.
Juni 24, 2017- Kamati ya Uchaguzi kutangaza majina ya wagombea waliostahili au waliotimiza taratibu za uchaguzi kwa mujibu wa katib au kanuni za TWFA.
Juni 26 na 27, 2017- Kupokea pingamizi kati ya saa 4:00 asubuhi hadi saa 10:00 jioni.
Juni 28, 2017- Kamati ya Uchaguzi kupitia pingamizi kama zimewasilishwa.
Juni 29, 2017-  Kamati kutoa majumuisho ya pingamizi kama ziliwasilishwa na wadau.
Juni 30, 2017-  Usaili kwa wagombea waliotangazwa
Julai 01, 2017- Kutangaza majina ya wagombea waliopitishwa
Julai 02, 2017-Kamati kupokea rufaa
Julai 03, 2017-  Kamati kupitia rufaa kama zimewasilishwa
Julai 04, 2017   Kamati kutangaza orodha ya mwisho ya wagombea
Julai 04 hadi 07, 2017-Wagombea kufanya kampeni kwa kuzingatia maadili
Julai 08, 2017- Uchaguzi Mkuu wa TWFA


Mushumba amesema kwamba nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu, Katibu Msaidizi, Mweka Hazina, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji. Sifa ya elimu kwa wagombea wote ni kidato cha nne.


Kwa nafasi ya Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu na Katibu Msaidizi fomu zitanunuliwa kwa Sh 200,000 wakati nafasi za Mweka Hazina, Mjumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF na Wajumbe wanne wa Kamati ya Utendaji fomu zitapoatikana kwa Sh 100,000. Fomu zitapatikana ofisi za Hosteli ya TFF zilizoko Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.

NENO KUTOKA KWA RAIS WA TFF KUELEKEA UCHAGUZI MKUU


Ndugu zangu viongozi, wapenzi na wadau wa mpira wa miguu Tanzania.


Kama ilivyotangazwa na kamati yetu ya uchaguzi leo tumeanza rasmi mchakato wa uchaguzi wetu.


Hiki ni kipindi muhimu kwa ustawi wa mpira wetu.


Ninaomba niwahakikishie wadau wa mpira wa miguu Tanzania kuwa Sekretarieti ya TFF ambayo kikatiba ninaisimamia mimi itaendelea na shughuli zake bila kuathiriwa na mchakato huu, hii itakuwa ni pamoja na kuandaa timu zetu mbalimbali za Taifa na kushughulikia majukumu yake mengine ya kila siku.


Aidha ninaomba niwahakikishie viongozi na wadau wa mpira wa miguu Tanzania kuwa mimi kama Rais wa TFF sina kundi katika uchaguzi huu.


Msimamo wangu ni kuwa wagombea wote wana haki sawa na sanduku la kura ndilo litaamua nani ataongoza mpira wetu kwa kipindi cha 2017-2021.


Wagombea wote ninawatakia kila la kheri na Mola awabariki na kuwaongoza.


Ahsanteni

Jamal Emil Malinzi

Rais wa TFF

TFF YARAHISISHA UPATIKANAJI FOMU ZA UCHAGUZI


Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), linapenda kuwatangazia wanafamilia wote wa mpira wa miguu wenye nia ya kuwania uongozi kuwa limewarahisishia namna ya kupata fomu baada ya tovuti ya TFF: www.tff.or.tz kuwa kwenye marekebisho.


Kwa wanafamilia ambao wapo nje ya Dar es Salaam, wanaotaka fomu hizo kwa sasa hawana budi kutuma ujumbe wa barua pepe kwenda kwenye anwani ya info@tff.or.tz na moja kwa moja atajibiwa kwa kupata fomu hizo ziliazoanza kutolewa leo Juni 16, mwaka huu. Kwa walioko Dar es Salaam, wanaweza kupata fomu hizo katika ofisi za TFF zilizo Karume, Ilala jijini Dar es Salaam.


Mwanafamilia wa mpira wa miguu mwenye nia ya kugombea ataweza kufungua fomu hizo na kuzijaza huku akifuata utaratibu wa kulipia kwenye nambari ya akaunti 01J1019956700 katika Benki ya CRDB.


Zoezi hili kuchukua fomu na kuzirejesha fomu lililoanza leo Juni 16, litafikia kikomo Juni 20, mwaka huu kwa mujibu wa Kanuni ya 10.8 ya Uchaguzi kama ilivyoanishwa kwenye katiba ya TFF.


Mara baada ya kulipia, Mgombea atawajibika kuwasilisha stakabadhi ya malipo kutoka benki na kupewa fomu ya nafasi husika.


Gharama za kuchukulia fomu ni.

1.   Rais TSHS 500,000/=

2.   Makamu wa Rais TSHS 300,000/=

3.   Wajumbe wa kamaki ya utendaji TSHS 200,000/=


RAIS MALINZI AMSHUKURU MGOYI


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania, Jamal Malinzi amempongeza Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa TFF, Ahmed Mgoyi kwa utumushi mara baada ya kutangaza kutowania nafasi yoyote ya uongozi.


Mjumbe Mgoyi anayewakilisha Mikoa ya Kigoma na Tabora aliandika waraka jana Juni 15, 2017 akielezea kutogombea tena katika Uchaguzi wa TFF unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu.


“Nimefanya kazi na Wajumbe wangu wote wa Kamati ya Utendaji. Tumefanya kazi kwa uadilifu mkubwa. Wakati Tukielekea kwenye uchaguzi, mwenzetu ametangaza kutogombea tena, lakini kwa namna nilivyofanya naye kazi, kwangu mimi naamini anahitajika mno, lakini uamuzi wake ni mwisho unakuwa ni wa kwao.


“Naamini kwamba bado ni mwanafamilia wa mpira wa miguu na pindi atakapohitajika kwa lolote lile kama vile ushauri na masuala mengine, basi hatutasita kuwafuata kwa sababu lengo ni kujenga na kuendeleza mpira wetu,” amesema Malinzi.


Katika ujumbe wake, Rais Malinzi amesema kwamba hadhani kama Mgoyi hao atasita au kukataa kutoa ushirikiano kwa uongozi wa shirikisho pindi akihitajika kutoa msaada wao wa mawazo na ushauri.


Rais Malinzi amemtakia kila la kheri katika majukumu yake mengine aliyojipangia kuyafanya huku akiwa bado mwanafamilia wa mpira wa miguu.

PONGEZI KWA FRANCIS AMIN MICHAEL


Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Emil Malinzi, amempongeza Francis Amin Michael kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Mpira wa Miguu cha Sudan Kusini (SSFA).


Amin - Mfanyabiashara aliyepata kuwa Mjumbe wa Bodi ya timu Atlabara FC, alishinda nafasi hiyo katika Uchaguzi Mkuu uliofanyika Juba ambako aliwashinda Lual Maluk Lual na Arop Joh Aguer baada ya kuvuna kura 22 kati ya 34.


Amin anamrithi Chabur Goc Alei, ambaye hakutetea nafasi hiyo.


Katika salamu za pongezi, Rais Jamal Malinzi amesema kwamba ana imani na Amin katika nafasi hiyo kwa kuwatumikia vema Wana Sudan Kusini kama alivyoahidi mara baada ya kuchaguliwa kushika wadhifa huo.


Rais Malinzi anaamini kwamba kwa kushirikiana na wadau mbalimbali kama vile Serikali ya Sudan Kusini, ataendeleza mpira wa miguu hususani katika Baraza la Mpira wa Miguu la Afrika Mashariki ambako Tanzania na Sudan Kusini ni nchi wanachama.

MGOYI ASEMA HATARAJII KUGOMBEA TENA UJUMBE WA KAMATI YA UTENDAJI TFF



Kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema na mwenye Ukarimu
 
TFF inaelekea kwenye Uchaguzi wake mwingine  ambao tunategemea kuundwa kwa safu nyingine ya Uongozi itakayoendeleza Gurudumu la Soka nchini.

Binafsi naomba kuchangia muda nanyi kuwasilisha *SHUKRANI* zangu za dhati kabisa kwa Wadau wote wa soka tulioshirikiana kwa njia moja ama nyingine katika kipindi chote cha miaka 13 ambacho nilichaguliwa na kuhudumu kama Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF kwenye chaguzi zote tatu nilizoshiriki ambapo kwa mara ya kwanza nikiingia nikiwa Mjumbe mwenye umri mdogo zaidi kuliko wote. Aidha kuomba radhi kwa mapungufu yoyote na yaliyotokana nayo kwa kipindi chote hicho:

Nawashukuru sana wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF katika Chaguzi tatu za TFF kuonyesha Imani na mimi na kunichagua kwa kishindo cha kura nyingi sana kwa nyakati zote hizo.

Naishukuru Kamati ya Utendaji ya TFF inayomaliza muda wake chini ya Rais Jamal Malinzi kwa ushirikiano uliotukuka na nitawakumbuka sana kwa mengi mchanganyiko.

Namshkuru binafsi Leodegar Chilla Tenga aliyenijenga kuwa Kiongozi imara wa Mpira.

Nawashukuru ma-Rais wote wawili niliofanya nao kazi (Tenga na Malinzi) makamu wao na Kamati zao za Utendaji kwa kuniamini kwa nyakati tofauti kunifanya kuwa msimamizi wa shughuli kadhaa miongoni mwa shughuli za TFF.

Navishukuru vyombo vya habari na wanahabari kwa ushirikiano wakati wote.

Naishukuru klabu mashuhuri, Wana Kinyamtula, Never say Die, The Uncolonized, Watoto wa Jiji,  *Ashanti United* niliyoingoza kama Meneja wa timu mpaka Rais wake kwa zaidi ya miaka 20 kwa kunisaidia sana kunijenga kiUongozi na kuniongezea Uthubutu.

Nawashkuru wadau wa Mpira wa Kigoma kwa kuniamini na kunifanya kuwa sehemu ya Uongozi wa Mpira.

Nawashukuru Vilabu vyote vya VPL, FDL, SDL na RCL kwa ushirikiano navyo kwa nyakati tofauti tofauti.

Nawashkuru wafanyakati wote wa TFF na timu za Taifa nilioshirikiana nao kwa nyakati tofauti.

Naishukuru sana Serikali na watendaji wa serikali kwa ushirikiano wakati wote.

Nawashkuru wadhamini na watendaji wa wadhamini wa TFF niliofanya nao kazi kwa nyakati tofauti.

Shukrani zangu zinatokana na yaliyopita na bado naendelea kuamini nitaendelea kushirikiana na nyanja zote kama sehemu ya familia ya Mpira wa Miguu.

Najisikia Fahari sana kuwa sehemu ya Ujenzi wa TFF katika mifumo thabiti na kuwa sehemu ya Usimamizi wa Mafanikio ya Mabadiliko Chanya ya Shuguli za TFF  bila ya kujali na kuthamini Changamoto za Utii na Uendeshaji zinazosababishwa na kutokana nazo.

Naomba kwa dhati kabisa na nikiendelea kuamini kwenye kuhuishwa na kuendelezwa na kufanywa kwa weledi zaidi kwa mema  yaliyopangwa na kufanywa na TFF kwa vipindi vyote nilivyokuwepo na wakati mwingine ikiwemo Ulinzi kwa Mifumo na Misingi ya kiTaasisi iliyowekwa,  Matumizi sahihi ya Vyombo vya TFF, Uthubutu na Mafanikio kwa Uendelezaji wa Soka la Vijana na Wanawake, Muundo wa Uendeshaji wa Mashindano yetu na Mafunzo.

Pamoja na kuwa bado nina nguvu uwezo na sifa za kuendelea kugombea, lakini pia nimeamini ni wakati wa kutoa nafasi pana zaidi kwa wengine kugombea na kuwa badala yangu na heshima kwa fikra nyinginezo. Na ninaondoka nikiwa mjumbe wa muda mrefu zaidi ya wote kwenye Kamati ya Utendaji inayokamilisha kipindi cha kikatiba na kwa dhati kabisa naamini kwenye kutoa nafasi kwa wengine.

Nawaomba radhi wale wote ambao wangependa au kutarajia ningekuwa miongoni au wakiendelea kuamini kuwa nilistahili kuwa sehemu ya wagombea.. nawashukuru kwa imani yao kwangu na bado nipo nao pamoja, pamoja na wale ambao hawaamini hivyo kama sehemu ya familia ya Mpira wa Miguu Tanzania na kwingineko.

Nawatakia kila la kheri wagombea wote na kwa nafasi na uzoefu wangu najishawishi kuamini kwamba wagombea wote watakuwa wamejipima vya kutosha na kuzihakiki dhamira zao, wamejiridhisha na wanavyoijua TFF, ukubwa wake na shughuli zake, wamefuatilia na kutambua vema mahitaji ya mpira wetu, wametathmini changamoto, madhaifu na makusudi ya kiuongozi na wapo tayari kwa mabadiliko, wametambua maeneo TFF inayofeli au hayajafanywa vema zaidi na wanaamini kwenye kuwa sehemu ya ufumbuzi, wamezikataza nafsi zao kufuata matamanio ya mapenzi ya timu zao, wanafahamu nguzo kuu za mpira wa miguu na changamoto zinazozikabili na namna ya kuzitatua, utayari wao kujitolea kwa hali na mali, kuheshimu miiko ya kiUongozi na kuimarisha nidhamu na Uadilifu.

Nimesukumwa kutoa Ushauri wangu huu kwa kuendelea kuathiriwa na kutoamini sana kwenye Utekelezaji na Udhibiti wa  kimfumo wa kupatikana kwa Viongozi wa Mpira hasa katika ngazi za juu kama hizi zinazokwenda kugombewa.

Kila la kheri Wagombea.
Ramadhani Kareem
Nawashukuru sana.
Ahmed Iddi Mgoyi
Mjumbe Kamati ya Utendaji TFF (Kigoma na Tabora 2004-2017)
13 Juni 2017.