KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, June 12, 2017

GOR MAHIA YATWAA UBINGWA KOMBE LA SPORTPESA, SASA KUCHEZA NA EVERTON JULAI 13- DAR


SportPesa imeanza kuthibitisha nia yake ya kendeleza soka la Tanzania kwa kutangaza kuwa mshindi wa michuano ya SportPesa Super Cup atawavaa miamba wa soka wa Uingereza, Everton. 

Hii itakuwa ni mara ya kwanza kwa klabu ya Ligi Kuu ya England kucheza na klabu ya soka ya Afrika Mashariki.

Tangazo hil limetolewa katika mkutano na waandishi wa habari uliofanyika wenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam uliohudhuriwa na Mkurugenzi Mtendaji wa SportPesa, Pavel Slavkov, Mkurugenzi wa Utawala wa SportPesa, Tarimba Abbas, Muu wa masoko wa Kimataifa, Joyce Kibe, Mkurugenzi Mtendaji wa Everton, Robert Elstone, Balozi wa Everton FC, Leon Osman, Waziri wa Michezo Dk. Harrison Mwakyembe, Murugenzi wa Michezo Yusuph Singo, Rais wa TFF Jamal Malinzi na wanahabari. Mechi hiyo inayosubiriwa kwa hamu itapigwa Julai 13 kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

SportPesa ilitangaza Mei 24 kwamba michuano ya SportPesa Super Cup itafanyika jijini Dar es Salaam kwenye Uwanja wa Uhuru ikishirikisha timu nne (4) za Tanzania dhidi ya timu nne (4) kutoka Kenya. Timu sita (6) kati ya zitakazoshiriki michuano hiyo ni klabu washirika rasmi wa SportPesa. Simba SC, Young Africans SC na Singida United FC ni washirika wa SportPesa Tanzania wakati Nakuru All Stars, AFC Leopards na Gor Mahia ni washirika wa SportPesa kutoka Kenya. 

Tusker FC ndiomabingwa wa Ligi Kuu ya SportPesa ya Kenya wakati Jang’ombe Boys FC ni vinara katika Ligi Kuu ya Zanzibar.

Akifurahia ujuio wa Everton, Mkurugenzi Mtendaji wa SportPesa, Pavel Slavkov alisema; “Tunafuraha kuwakaribisha Everton nchini Tanzania, ziara yao itakuwa na manufaa siyo tu kwa klabu za hapa zitakazopata fursa ya kucheza na mabingwa hao mara 9 wa Ligi Kuu ya England, bali pia na taifa zima kwa ujumla.

“Katika ziara hiyo tutashirikiana kufanya shughuli kadhaa za kurudisha kwa jamii.

“Tanzania inapaswa kujiandaa kupata uzoefu  mkubwa kutokana na uwepo wa Everton mjini hapa.”

Robert Elstone, Mkurugenzi Mtendaji wa Everton alisema: “Maandaizi ya mwanzo wa msimu mpya ni kipindi muhimu sana kwetu kwani kwa kocha Ronald Koeman na benchi lake la ufundi wakiwaandaa wachezaji kwa ajili ya msimu mkubwa ujao. Kuwa timu ya kwanza ya Ligi Kuu ya England kuja kucheza Tanzania itakuwa ni sehemu muhimu ya maandalizi hayo.

“Tunafungua milango mipya na hatuna shaka kwamba tutapata marafiki na kuongeza mashabiki wetu kkmataifa tutakapokuja Julai.

“Najua Ronald Koeman na wachezaji wanajiandaa kuja kucheza mechi nzuri dhidi ya moja ya klabu bora ya Afrika Mashariki.”

SportPesa tangu ilipozinduliwa Tanzania Mei 9, 2017, imethibitisha nia yake ya kufanya mapinduzi ya soka nchini hapa kwa kuzidhamini klabu tatu za soka, ikichangia Sh. Milioni 50 za Kitanzania katika kuisapoti timu ya taifa ya vijana ya U-17 Serengeti Boys ambayo ilikuwa ikishiriki michuano ya AFCON ya vijana nchini  Gabon, imetangaza michuano ya SportPesa Super Cup ambayo inaweza kuwakutanisha miamba wa soka wa Tanzania, Yanga na Simba katika nusu-fainali /au fainali, na pia kumshuhudia bingwa wa Kombe la SportPesa akiwavaa miamba hao wa Uingereza.

No comments:

Post a Comment