KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Tuesday, December 11, 2012

BREAKING NEWS, YANGA, AZAM, SIMBA ZAPATA PIGO, ZFA YAWAFUNGIA WACHEZAJI WOTE WA ZANZIBAR HEROES



CHAMA cha Soka cha Zanzibar (ZFA) kimewafungia kwa muda usiojulikana wachezaji wote wa timu
ya Zanzibar, Zanzibar Heroes iliyoshiriki katika michuano ya Kombe la Chalenji iliyomalizika mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Kampala, Uganda.
Mjumbe wa kamati ya utendaji ya ZFA, Mussa Soraga ameiambia blogu ya liwazozito jioni hii kuwa, uamuzi huo umefikiwa katika kikao cha dharula cha kamati hiyo kilichoitishwa na Mwenyekiti, Amani Makungu.
Soraga alisema ZFA imefikia uamuzi huo, kufuatia kitendo cha nahodha wa Zanzibar Heroes, Nadir Haroub Cannavaro kumnyang'anya dola 10,000 Katibu Mtendaji wa chama hicho, Kassim Ally na kuzigawa kwa wachezaji.
Kwa mujibu wa Soraga, fedha hizo ni zile zilizotolewa na Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na Kati (CECAFA) kutokana na Zanzibar kushika nafasi ya tatu katika michuano ya Kombe la Chalenji.
Soraga alisema baada ya Cannavaro kumnyang'anya Kassim fedha hizo, aliamua kuzigawa kwa wachezaji kwa madai kuwa ni mali yao na si ya ZFA.
Mjumbe huyo wa ZFA alisema kutokana na kitendo cha wachezaji kukubali kugawana fedha hizo, chama hicho kimewaona wote kuwa wana hatia ya kushiriki kula njama ya kupora fedha hizo na
kugawana.
"Kitendo kilichofanywa na wachezaji wetu ni cha aibu na kimeifedhehesha mno serikali ndio sababu ZFA iliamua kukutana kwa dharula leo na kuamua kuchukua uamuzi huu mzito,"amesema Soraga alipozungumza na liwazozito muda mfupi uliopita.
Kutokana na uamuzi huo, Soraga alisema chama chake kimeamua kuandika barua kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kulifahamisha kwamba, wachezaji hao, waliopo kwenye timu ya taifa, Taifa Stars na klabu za Yanga, Azam na Simba hawaruhusiwi kuzichezea kwenye michuano yoyote.
Wachezaji waliopo Tanzania Bara waliokumbwa na adhabu hiyo ni Cannavaro wa Yanga, Aggrey Morris na Samir Nuhu wa Azam, Selemani Selembe wa Coastal Union na Masoud Nassoro Cholo na Twaha wa Mtibwa Sugar.

No comments:

Post a Comment