Rais Jakaya Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na wasanii waliomtembelea Ikulu, Dar es Salaam
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha Muziki wa Dansi nchini, Addo Mwasongole
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na mwanamuziki nyota wa zamani wa bendi ya Mlimani Park, Cosmas Thobias Chidumume
Rais Jakaya Kikwete akiteta jambo na mwanamuziki nyota wa Injili, Flora Mbasha na mumewe.
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na kiongozi wa bendi ya Bantu Group na mpiga gita la solo mahiri nchini, Hamza Kalala 'Komandoo'
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na mwanamuziki mkongwe mwenye asili ya DRC, Kikumbi Mwanza Mpango Mwema Kikii
Rais Jakaya Kikwete akionekana kufurahia jambo na msanii wa muziki wa kizazi kipya, Khamis Mwinjuma 'Mwana FA'
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na msanii wa muziki wa kizazi kipya, Khamis Mwinjuma 'Mwana FA'
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na mwanamuziki Abdul Salvador
Rais Jakaya Kikwete akisalimiana na mwimbaji mkongwe wa taarab nchini, Shakila Saidi, ambaye anaimbia kundi la JKT
RAIS Jakaya Kikwete akisalimiana na mwanamuziki mkongwe, Waziri Ally wa bendi ya The Kilimanjaro 'Wana Njenje'
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARISerikali imeanza kutoa Nishani kwa wasanii kwa vile inatambua umuhimu wao katika jamii.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewaeleza wawakilishi wa sanaa mbalimbali nchini waliofika Ikulu leo asubuhi kutoa shukrani kwa Mheshimiwa Rais kwa kuwatambua na kuwapa heshima kubwa ya Tuzo na Nishani wasanii katika siku ya sherehe za Uhuru za tarehe 9 Disemba, Ikulu, Dar-Es-Salaam.
“Tumetoa Nishani kwa vile wasanii wanatoa mchango mkubwa, tumeanza kutoa nishani mwaka huu na tutaendelea kutoa miaka ijayo kwani kwa kuitambua sanaa, mnawapa moyo wasanii kuendelea kujituma na kuwa wabunifu zaidi” Rais amesema na kuongeza, “Tumeingiza Nishani ya Wasanii na Watafiti maana nao wanafanya kazi kubwa sana ya kutafiti mazao na mbegu mbalimbali ambazo zinaongeza tija katika kilimo nchini”.
Katika kumbukumbu ya kusherehekea miaka 51 ya Uhuru wa Tanzania bara mwaka huu, Rais Kikwete alitunuku nishani kwa makundi mbalimbali ya watu waliotoa mchango mkubwa katika jamii na waliotumikia taifa kwa uadilifu.
Rais alitoa Nishani ya Sanaa na Michezo kwa mara ya kwanza kwa wasanii nchini ambapo Bi. Fatma Baraka Khamis (Bi Kidude) kupitia Baraza la Sanaa Zanzibar, Kiongozi wa Muziki wa Dansi ya Msondo Ngoma Muhidin Maalim Gurumo, Kiongozi wa Zamani wa Bendi ya Dar Intrenational Marehemu Marijan Rajab walipata tuzo hiyo.
Wengine ni Msanii wa maigizo na filamu nchini Marehemu Fundi Said (Mzee Kipara) na Mwanariadha mkongwe John Steven Akwari.
Rais amewataka wasanii kushirikiana na serikali lakini pia wawe mstari wa mbele katika kupigania haki zao na sio kusubiri serikali tu iwafanyie hivyo.
Wasanii hao wamefika Ikulu wakiongozwa na Bw. Ruge Mutahaba wa Clouds Media Group.
Wengine ni Addo Mwasongwe, Rais wa Shirikisho la Muziki na Mwenyekiti wa Chama cha Muziki wa Injili, Bw. Juma Ubao Mwenyekiti wa Chama cha Muziki Tanzania (CHAMUDATA), aliyewakilishwa na Hamza Kalala.
Bibi Shakila Said, Mkongwe wa Muziki wa Taarab Nchini, Bi Carola Kinasha Msanii wa Muziki , Mzee King Kiki msanii wa Muziki wa Dansi Mwana FA, msanii wa Kizazi Kipya na Bw. Waziri Ally , msanii wa Muziki.
Wawakilishi hao pia wamemshukuru Rais kwa msaada wa hali na mali anaotoa kwa wasanii mbalimbali wanapopata matatizo ambao hivi sasa wapo katika hatua mbalimbali za matibabu ya afya zao hapa nchini na nchi za Nje.
“Haya mengine ninayafanya tukama wajibu wa kibinadamu kwa vile nina nafasi ya kufanya hivyo na pale tunapokua na uwezo tunasaidia kama binadamu wenzetu” Rais Amesema.
Imetolewa na Premi Kibanga,
Mwandishi Habari wa Rais, Msaidizi,
Ikulu - DSM
21 Desemba, 2012
No comments:
Post a Comment