KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, December 3, 2012

KOMBE LA UHAI KUANZA DES 7



Michuano ya Kombe la Uhai inayoshirikisha timu za U20 za klabu za Ligi Kuu ya Vodacom inatarajia kuanza Desemba 7 mwaka huu na kumalizika Desemba 22 mwaka huu.

Wachezaji watakaoshiriki michuano hiyo ni wale tu ambao usajili wao umefanyika Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) na kupata leseni.

Hakutakuwa na usajili  mwingine wowote mbali na ule uliofanyika sambamba na wa Ligi Kuu.

Taratibu zote za michuano hiyo zitafahamishwa kwa klabu husika ikiwemo ratiba ya michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment