KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Saturday, December 1, 2012

SERENGETI BOYS YAFUNGISHWA VIRAGO NA CONGO BRAZAVILLE



TIMU ya soka ya taifa ya vijana wa chini ya miaka 17, Serengeti Boys imetolewa katika michuano ya kuwania kufuzu kucheza fainali za Afrika baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Congo Brazaville katika mechi ya marudiano ya raundi ya tatu iliyochezwa mjini Brazaville.
Kipigo hicho kimeifanya Serengeti Boys itolewe kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-1, kufuatia kushinda bao 1-0 katika mechi ya awali iliyopigwa wiki mbili zilizopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mechi hiyo ilitawaliwa na matukio mengi ya vurugu yaliyofanywa na wenyeji kwa lengo la kuwavuruga wachezaji wa Serengeti Boys kisaikolojia.
Katika moja ya matukio hayo, Kocha Msaidizi wa Serengeti Boys, Jamhuri Kihwelo alipigwa na polisi wa Congo wakati mpira ukiendelea.
Serengeti Boys inatarajiwa kurejea nchini leo.

No comments:

Post a Comment