KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, December 20, 2012

TFF YAITEGA ZFA



Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limepokea barua ya Chama cha Mpira wa Miguu Zanzibar (ZFA) ikieleza kuwafungia wachezaji kadhaa Wazanzibari wanaochezea klabu mbalimbali za timu za Tanzania Bara na timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars).

Suala hilo limepelekwa kwa Kamati ya Nidhamu na Usuluhishi ya TFF kwa hatua zaidi, hivyo kwa sasa Shirikisho litasubiri uamuzi wa kamati hiyo.

Baadhi ya wachezaji hao ni nahodha msaidizi wa Taifa Stars, Aggrey Morris, Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Nassoro Masoud Cholo, Mcha Khamis, Seif Abdallah na Selemani Kassim Selembe.

No comments:

Post a Comment