KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, December 6, 2012

MKUTANO WA WANACHAMA YANGA MWAKANI



KLABU ya Yanga imeahirisha mkutano wake wa wanachama uliopangwa kufanika kesho makao makuu ya klabu hiyo mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.
Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana na Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji imeeleza kuwa, mkutano huo sasa utafanyika Januari 19, 2013.
Manji amezitaja sababu za kusogezwa mbele kwa mkutano huo kuwa ni kutoa nafasi kwa wanachama na wapenzi wa Yanga kushiriki kikamilifu katika maandalizi ya sherehe za Uhuru wa Tanzania Bara, zitakazofanyika Jumapili.
Aliitaja sababu nyingine kuwa ni klabu hiyo kuwa na mazungumzo na kampuni moja maarufu nchini kwa ajili ya kusimamia shughuli za mkutano huo kwa upande wa ufadhili.
Alisema kampuni hiyo imeomba iongezewe muda ili iweze kufanyakazi hiyo kwa ufanisi, ambapo lengo ni kutunisha mfuko wa klabu kwa kuiingizia kati ya sh. milioni 200 hadi sh. milioni 350.
Manji amewashukuru wanachama na wapenzi wa Yanga kwa kuendelea kuwa na mshikamani uliopo sasa na kuwataka wazidi kuijenga klabu hiyo ili iweze kupata mafanikio zaidi.

No comments:

Post a Comment