Uongozi wa Azam Academy umejigamba kuwa, umepania kuhakikisha timu ya vijana wa chini ya umri wa miaka 20 inatwaa kombe la Uhai.
Michuano hiyo inayodhaminiwa na kampuni ya Said Salim Bakhresa itakutanisha timu zote 14 zinazoshiriki ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2012/2013 na inafanyika kwenye viwanja vya Kumbukumbu yaKarume na Azam Stadium Chamazi jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na tovuti ya www.azamfc.co.tz kocha msaidizi wa Azam Academy, Iddi Cheche amesema kikosi hichokimejiandaa na kipo tayari kushindana na kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.
“Mwaka huu tumejiandaa vizuri, timu iko imara kwa maandalizi ya kutosha tofauti na mwaka jana, tunauhakika wakutwaa ubingwa japo mashindano yatakuwa magumu” alisema kocha Cheche.
Aliongeza kuwa wameziba mapengo yalijitokeza katika mashindano yaliyopita kwa kuwapa mafunzo zaidi vijana waoili kwenda sawa na mashindano hayo.
Kombe la Uhai lilianzishwa mwaka 2008, ambako Azam Academy ilitwaa kombe hilo mwaka 2009 na 2009, 2010kombe hilo likachukuliwa na Ruvu Shooting na mwaka jana lilienda kwa Simba B
Wakati huo huo, Brian Umony, mshambuliaji bora wa Uganda na Afrika Mashariki kwa sasa, ambaye jusi alitwaa tuzo ya mchezaji bora wa CECAFA ametua Azam FC
Umony Mchezaji wa zamani wa Supersports United ya Afrika ya kusini na Portland Timber ya New England ya Marekani amejiunga na Azam FC kwa mkataba wa miaka miwili
No comments:
Post a Comment