KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, December 9, 2012

UGANDA BINGWA CHALENJI, Z'BAR YA TATU



ZANZIBAR jana ilitwaa nafasi ya tatu katika michuano ya soka ya Kombe la Chalenji baada ya kuichapa Tanzania Bara kwa penalti 6-5 katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Namboole mjini Kampala, Uganda.

Timu hizo zililazimika kupigiana penalti tano tano baada ya kumaliza dakika 90 zikiwa sare ya bao 1-1.

Tanzania Bara ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 10 lililofungwa na Mwinyi Kazimoto kabla ya Abdalla Othman kuisawazishia Zanzibar dakika tano kabla ya mchezo kumalizika.

Uganda ilifanikiwa kutetea taji lake baada ya kuifunga Kenya mabao 2-1, ambayo yote Kenya walijfunga kupitia kwa wachezaj wao Anthony Kimani na Joackins Atudo. Bao la Kenya lilifungwa na Edwin Lavatsa.

No comments:

Post a Comment