KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Saturday, January 12, 2013

URAIS TFF SH. 500,000, FOMU KUANZA KUTOLEWA J'TATU

SHIRIKISHO la Soka Tanzania(TFF) limesema, fomu za kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika uchaguzi mkuu wa shirikisho hilo unaotarajiwa kufanyika Februari 24 mwaka huu, zitaanza kutolewa Jumatatu.

Taarifa iliyotolewa na TFF kwa vyombo vya habari jana ilisema kuwa, fomu hizo zinapatikana kwenye ofisi ya katibu mkuu wa shirikisho hilo kuanzia saa tatu asubuhi hadi saa10 jioni na mwisho wa kuzirejesha ni Januari 18 mwaka huu.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, nafasi zitakazogombewa katika uchaguzi huo ni ya rais, makamu wa rais na wajumbe wa kamati ya utendaji, ambapo nafasi zitakazogombewa ni 13.

Taarifa hiyo iliongeza kuwa, ada ya fomu kwa wagombea wa nafasi ya urais ni sh. 500,000, wagombea wa nafasi ya makamu wa rais sh. 300,000 na wagombea wa nafasi ya wajumbe wa kamati ya utendaji sh. 200,000.

Imezitaja sifa za wagombea kuwa ni wawe raia wa Tanzania, kiwango cha elimu kisichopungua kidato cha nne, uzoefu wa uendeshaji wa soka, wasiwena hatia ya makosa ya jinai, umri uziopungua miaka 25,wawe wamewahi kucheza soka, makocha, waamuzi au kuendesha soka katika ngazi zozote.

Taarifa hiyo ilizitaja sifa za wagombea wa nafasiya rais na makamu wake kuwa ni kuwa na shahada ya chuo kikuu na uwezo wa kuwakilisha TFFndani na nje ya nje.

Wakati huo huo, fomu za kuwania uongozi wa Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, uliopangwa kufanyika Februari 22 mwaka huu, zitaanza kutolewa Jumatatu.

Nafasi zitakazogombewa katika uchaguzi huo ni ya mwenyekiti wa bodi, makamu mwenyekiti, wajumbe wawili wa kuziwakilisha klabu za ligi daraja la kwanza kwenye kamatiya uongozi.

Ada ya fomu kwa wagombea wa nafasi ya mwenyekiti ni sh. 200,000 wakati wagombea wa nafasi za ujumbe watalipa sh. 100,000.

No comments:

Post a Comment