KLABU ya Azam imejigamba kuwa, nyota wake wapya waliosajiliwa kwa ajili ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya Tanzania Bara, wametoa mchango mkubwa kwa timu hiyo katika michuano ya Kombe la Mapinduzi.
Kocha Msaidizi wa timu hiyo, Kalimagonga Ongara ameieleza tovuti ya Azam jana kuwa, huo ni mwanzo mzuri kwa wachezaji hao kutokana na kumudu vyema nafasi wanazocheza.
Wachezaji wapya waliosajiliwa na Azam wakati wa usajili wa dirisha dogo ni Brian Umony kutoka Uganda, Jockins Atudo na Humphrey Mieno kutoka Kenya, David Mwantika kutoka Prisons, Seif Abdallah kutoka JKT Oljoro na Uhuru Selemani kutoka Simba.
"Wachezaji hawa wameonyesha umahiri mkubwa wa kucheza soka na hii ni ishara nzuri kwa Azam kwamba itakuwa tishio zaidi katika mzunguko wa pili wa ligi kuu,"alisema.
Ongara alisema anaamini kadri siku zinavyokwenda mbele, wachezaji hao wapya watazidi kuelewana vyema na wenzao wa zamani na kuifanya Azam itimize malengo yake ya kutwaa ubingwa wa bara.
No comments:
Post a Comment