KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, January 3, 2013

SIMBA YAANZA VYEMA KOMBE LA MAPINDUZI


SIMBA jana ilianza vyema michuano ya soka ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuichapa Jamhuri ya Pemba mabao 4-2 katika mechi ya ufunguzi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Pambano hilo halikuwa na mvuto sana kwa mashabiki kutokana na kuathiriwa na mvua iliyoanza kunyesha kabla ya timu kuingia uwanjani na hivyo kuwafanya wachezaji wateleze.

Jamhuri ilikuwa ya kwanza kupata bao dakika ya 17 kupitia kwa Mfanyeje Mussa Yussuf kabla ya Haruna Chanongo kuisawazishia Simba dakika ya 27.

Dakika mbili baadaye Simba iliongeza bao la pili kupitia kwa Chanongo kabla ya Mfanyeje kuisawazishia Jamhuri na kuzifanya timu hizo ziende mapumziko zikiwa sare ya mabao 2-2.

Simba iliongeza makali ya mchezo katika kipindi cha pili na kufanikiwa kuongeza mabao mengine mawili kupitia kwa Felix Sunzu na Shomari Kapombe.

No comments:

Post a Comment