KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, January 10, 2013

MKUTANO YANGA SASA JAN 20

UONGOZI wa klabu ya Yanga umeamua kusogeza mbele kwa siku moja tarehe ya mkutano mkuu wa wanachama wa klabu hiyo, uliopangwa kufanyika Januari 19 mwaka huu.

Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako alisema mjini Dar es Salaam jana kuwa, mkutano huo sasa utafanyika Januari 20 mwaka huu.

Mwalusako alisema wameamua kusogeza mbele tarehe ya mkutano huo ili kutoa nafasi kwa wanachama kufanya maandalizi, ikiwa ni pamoja na kulipia kadi zao.

Alisema uamuzi huo umefanyika baada ya uongozi kubaini kuwa, baadhi ya wanachama watashindwa kuhudhuria mkutano huo iwapo utafanyika siku ya Jumamosi kwa vile watakuwa kazini.

Katibu Mkuu huyo wa Yanga alisema, siku ya Jumapili ni nzuri zaidi kwa wanachama kufika mkutanoni kwa vile ni siku ya mapumziko kikazi.

Amewataka wanachama wa klabu hiyo kujitokeza kwa wingi kulipia kadi zao za uanachama ili waweze kuwa na haki ya kushiriki katika mkutano huo, ambao alisema utajadili mambo mengi muhimu.

No comments:

Post a Comment