KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, August 16, 2012

OMOTOLA ATOKA 'OUT' NA MUMEWE

LAGOS, Nigeria
HAKUNA wasiwasi kwamba mcheza filamu Omotola Jalade-Ekeinde ni mzuri kwa sura na hata umbo. Ni mmoja wa waigizaji wenye mvuto nchini Nigeria, sio tu kwa sababu ya uzuri wake, bali pia uigizaji wake.
Si rahisi kuamini kwamba Omotola ni mama wa watoto wanne kutokana na umbile lake. Anaonekana kama vile bado mbichi au kama kuzaa, basi amezaa mtoto mmoja au wawili.
Bahati nyingine aliyonayo Omotola ni kwamba mumewe, Matthew Ekeinde naye ana sura yenye mvuto na ni rubani wa ndege, ambaye amekuwa akisafiri mara kwa mara.
Kutokana na majukumu ya kazi zao, ni nadra kwa Omotola na Ekeinde kutoka matembezini pamoja. Mara nyingi mmoja akiwa nyumbani, mwingine anakuwa mahali fulani kikazi.
Hali hiyo imesababisha mara nyingi Omotola ahudhurie hafla mbali mbali bila ya kuwa na mumewe, hali ambayo imekuwa ikizua maswali mengi kutoka kwa mashabiki wa filamu nchini Nigeria.
Lakini hivi karibuni, wanandoa hao walionekana wakiwa pamoja katika hafla ya uzinduzi wa filamu mpya ya Omotola, inayojulikana kwa jina la Last Flight To Abuja.
Katika hafla hiyo, Omotola na mumewe, ambao wamedumu kwenye ndoa kwa miaka 16, walikuwa kivutio kikubwa kwa vile ilikuwa mara yao ya kwanza kuonekana wakiwa pamoja na walivutia mno kwa mavazi.
Mvuto wao uliwafanya mapaparazi wengi wawe bize kuchukua picha zao. Nao hawakuwa na ajizi. Walisimama pamoja kwa muda mrefu ili kuwapa nafasi mapaparazi hao watekeleze majukumu yao.

No comments:

Post a Comment