KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, August 12, 2012

NGORONGORO HEROES YATOLEWA NA NIGERIA

TIMU ya soka ya taifa ya vijana wa chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes imetolewa katika michuano ya kuwania ubingwa wa Afrika baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Nigeria katika mechi ya marudiano iliyochezwa mjini Ilorin, Kwara, nigeria.

Kipigo hicho kimeifanya Ngorongoro Heroes itolewe kwa jumla ya mabao 4-1, kufuatia kuchapwa mabao 2-1 katika mechi ya awali iliyochezwa wiki mbili zilizopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Nigeria ilijipatia mabao yote mawili katika kipindi cha pili, moja likiwa kwa njia ya penalti.

Kwa ushindi huo, Nigeria imefuzu kucheza raundi ya tatu na ya mwisho kabla ya fainali za Afrika kwa vijana wenye umri chini ya miaka 20 zitakazofanyika mwakani nchini Algeria.

Nigeria sasa itakutana na mshindi kati ya Congo Brazzavile na Afrika Kusini.

No comments:

Post a Comment