KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, August 16, 2012

AZAM YAKANA KUMUUZA REDONDO

KLABU ya Azam imesema haijafikia makubaliano yoyote na klabu ya Simba kuhusu usajili wa mshambuliaji Ramadhani Chombo Redondo.
Akizungumza mjini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa Azam, Idrissa Nassoro alisema si kweli kwamba wamekubaliana na Simba kumuuza mchezaji huyo kwa sh. milioni 50.
“Sisi tunachotambua ni kwamba Redondo bado ni mchezaji wetu halali kwa sababu mkataba wake utamalizika mwakani na wala hatujafikia makubaliano yoyote na Simba,”alisema.
Azam imeelezea msimamo wake huo baada ya baadhi ya vyombo vya habari kuripoti juzi kuwa, wamekubaliana na Simba kumuuza mshambuliaji huyo kwa sh. milioni 50.
Simba ilitangaza kumsajili Redondo wiki mbili zilizopita baada ya mchezaji huyo kudai kuwa, mkataba wake na Azam ulishamalizika tangu Juni mwaka huu.
Hata hivyo, Azam imekuwa ikipinga usajili huo kwa madai kuwa, mkataba wao na Redondo utamalizika Juni mwaka 2013.
Kwa mujibu wa Idrisa, tayari klabu yake imeshawasilisha usajili wake kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), likiwemo jina la Azam.
Jana ilikuwa siku ya mwisho kwa timu zote 14 zitakazoshiriki kwenye ligi hiyo kuwasilisha usajili wake TFF. Hadi juzi, Azam na Kagera Sugar ndizo pekee zilizokuwa zimewasilisha usajili wake TFF.

No comments:

Post a Comment