KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, August 15, 2012

YANGA YAWASILISHA USAJILI WAKE TFF

Hatimaye klabu ya Yanga leo imewasilisha usajili wake wa wachezaji kwa ajili ya msimu ujao wa ligi kwa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF).

Yanga imewasilisha usajili huo leo saa 11 jioni, ikiwa ni saa chache kabla ya kumalizika kwa muda wa usajili kwa timu za ligi kuu.

Katibu Mkuu wa Yanga, Celestine Mwesigwa amesema wameamua kusajili wachezaji 28 badala ya 30 ili kutoa nafasi ya kuongezwa wengine wawili wapya wakati wa dirisha dogo.

Alisema iwapo benchi la ufundi litaona umuhimu wa kuongeza wachezaji wengine kwenye dirisha dogo, litafanya hivyo na pia kama litaona umuhimu wa kupunguza baadhi yao kutokana na kuonyesha kiwango duni, halitasita kufanya hivyo.

Katika usajili huo, Yanga imewasilisha majina ya mabeki Kevin Yondan na Mbuyi Twite, ambao pia walikuwa wakiwaniwa na klabu ya Simba.

Katika usajili huo, Yanga imeamua kuwahamishia kwenye kikosi cha pili wachezaji Frank Dumayo na Saimon Msuva, lakini itakuwa ikiwatumia katika mechi mbali mbali za kikosi cha kwanza.

Kikosi kamili kilichosajiliwa na Yanga ni kama ifuatavyo:
Walinda Mlango:
Yaw Berko, Ally Mustafa 'Barthez' na Said Mohamed
Walinzi wa pemebeni:Shadrack Nsajigwa, Godfrey Taita, Juma Abdul, Oscar Joshua, David Luhende na Stephano Mwasika
Walinzi wa kati:Nadir Haroub 'Cannavaro', Kelvin Yondan, Mbuyu Twite, Ibrahim Job na Ladislaus Mbogo
Viungo wa ulinzi:Athuman Idd 'Chuji', Juma Seif Kijiko na Salum Telela
Viungo wa pembeni:Nizar Khalfani, Shamte Ally, Idrisa Rashid na Omega Seme
Viungo washambuliaji:Haruna Niyonzima, Rashid Gumbo na Nurdin Bakari
Washambuliaji:Said Bahanaunzi, Hamis Kiiza 'Diego', Didier Kavambagu na Jeryson Tegete
Kikosi cha U-20 kina jumla ya majina ya wachezaji 22 ambao ni:
Walinda Mlango:
Geofrey Nyalusi na Yusuf Abdul
Walinzi: Said Manduta, Zuberi Juma, Said Mashaka, Benson Michael, Issa Ngao, Rashid Said
Viungo: Frank Domayo, Omary Nasry, Clever Charles, Mwinyi Bakari, Mpenda Abdallah
Washambuliaji wa pembeni: Abdulahman Ally, Hussein Moshi, Abdallah Salum, Rehani Kibingu
Washambuliaji: Saimon Msuva, George Banda, Notikely Masasi, Suleiman Ussi, Kassim Jongo

No comments:

Post a Comment