KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, August 15, 2012

STARS YATOKA SARE NA BOTSWANA

Mshambuliaji wa Taifa Stars,Mrisho Ngassa (8) akitafuta namna ya kuweza kumpita beki wa timu ya Botswana, Zebras Oscar Neenga wakati wa mechi Kirafiki ya Kimataifa iliyochezwa jana kwenye Uwanja wa Molopolole mjini Gaborone Bostwana, timu hizo zilitoka Sare ya kufungana mabao 3-3.

Mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania "Taifa Stars", Mrisho Ngassa akijaribu kutaka kumtoka beki wa timu ya taifa ya Botswana,Zebras Edwin Elerile wakati wa mechi ya Kimataifa ya Kirafiki iliyochezwa kwenye Uwanja Molepolole nje kitogo ya jijini la Gaborone.timu hizo zilitoka Sare ya kufungana mabao 3-3.Mabeki wa timu ya taifa "taifa stars" wakimwangilia mshambuliaji wa timu ya taifa ya Botswana akifunga bao la tatu wakati wa mechi ya kirafiki iliyochezwa jana kwenye uwanja wa Molepolole mjini Gaborone.


TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars imelazimisha sare ya kufungana mabao 3-3 na wenyeji Botswana mjini Gaborone katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa ulio kwenye kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA).
Katika mchezo huo, mabao ya Stars yalifungwa na Mwinyi Kazimoto, Erasto Nyoni ambaye baadaye alitolewa nje kwa kadi nyekundu na Mrisho Ngassa.

Stars inatarajiwa kurejea Dar es Salaam kesho baada ya mechi hiyo, na wachezaji wa timu hiyo kujiunga na klabu zao, kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.

SOURCE: BIN ZUBEIRY

No comments:

Post a Comment