KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, August 9, 2012

SUSAN: MIMI SI MSAGAJI

LAGOS, Nigeria
MCHEZA filamu Susan Peters wa Nigeria ameamua kuvunja ukimya kwa kukanusha madai kwamba amekuwa akijihusisha vitendo vya mapenzi ya jinsia moja.
Susan ameueleza mtandao wa naijerules hivi karibuni kuwa, amekuwa akikerwa na uvumi huo kwa sababu hauna ukweli wowote kwake.
Katika siku za hivi karibuni, baadhi ya vyombo vya habari vya Nigeria vimekuwa vikiripoti kuwa, mwana dada huyo amekuwa ‘akiwasaga’ wanawake wenzake.
“Mimi si msagaji. Kamwe sijawahi kujihusisha na vitendo hivi. Watu wanaonifahamu wanaelewa kwamba Susan Peters si msagaji,”alisema mwanadada huyo.
“Inawezekana uvumi huo umetokana na umbile langu lilivyojazia. Mwili wangu umejazia kwa sababu nimekuwa nikifanya sana mazoezi ya michezo mbali mbali,”aliongeza.
Aliitaja michezo, ambayo amekuwa akishiriki kuicheza kuwa ni mpira wa kikapu, gofu na kukimbia.
Hata hivyo, Susan alisema aliacha kucheza michezo hiyo kutokana na mwili wake kuendelea kujazia mithili ya mtu anayenyanyua vyuma.
“Kama nitarejea tena kwenye gym hivi sasa, mwili wangu utazidi kujazia, lakini mimi si msagaji. Watu waache kunizuishia vitu wasivyokuwa na uhakika navyo,”alisema.
Susan alisema anapenda kufanya mapenzi yanayowahusisha mwanamke na mwanaume, lakini kamwe sio ya watu wa jinsia moja.
Alisema anao marafiki wengi wa kike, lakini pia anao marafiki wengi zaidi wa kiume. Pia alisema anaye rafiki wa kiume (mpenzi).

No comments:

Post a Comment