KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, August 20, 2012

LIGI KUU Z'BAR KUANZA SEPT 8

Ligi Kuu ‘Grand Malt’ Sept 8. Itatanguliwa na ngao ya hisani Sept. mosi Na Salum Vuai, MaelezoCHAMA cha Soka Zanzibar (ZFA), kimetangaza Septemba 8, mwaka huu, kuwa ndiyo siku itakayofunguliwa pazia la ligi kuu ya soka Zanzibar inayodhaminiwa kupitia kinywaji cha ‘Grand Malt’.
Uamuzi huo umefikiwa jana, baada ya mkutano wa kamati tendaji ya chama hicho, uliofanyika katika ukumbi wa Bahari hoteli ya Zanzibar Ocean View.
Akitoa taarifa baada ya mkutano huo, Mjumbe wa kamati hiyo Mussa Suleiman Soraga, alisema patashika hizo zitatanguliwa na mchezo wa kuwania ngao ya hisani utakaozikutanisha bingwa wa msimu uliopita na makamu wake, Super Falcon na Jamhuri.
Alisema mechi hiyo, imepangwa kuchezwa Septemba 1, mwaka huu katika uwanja wa Amaan wakati wa saa 2:00 usiku, ambapo chama hicho kinakusudia kumualika Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Ali Iddi, kuwa mgeni rasmi.
Aliongeza kuwa, hafla ya kuzikabidhi vifaa timu zote 12 kwa ajili ya ligi kuu, itafanyika Agosti 25, katika hoteli ya Zanzibar Ocean View, mnamo saa nne asubuhi, ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk.
Soraga amezitaka klabu zote zitakazoshiriki ligi hiyo, zihudhurie katika hafla hiyo kwa kuwakilishwa na mameneja au makatibu wao, au viongozi wengine watakaowachagua.

No comments:

Post a Comment