KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, August 19, 2012

MREMBO WA CHINA ATWAA TAJI LA DUNIA



Mrembo wa China, Yu Wenxia leo ametwaa taji la mrembo wa dunia wa mwaka 2012 baada ya kuwabwaga washiriki wenzake zaidi ya 100 katika shindano lililofanyika mjini Sanya, China.


Katika shindano hilo, mrembo kutoka Wales, Sophie Elizabeth Moulds aliibuka mshindi wa pili wakati mrembo wa Australia, Jessica Michell Kahawaty alishika nafasi ya tatu.

Hii ni mara ya pili kwa mrembo kutoka China kutwaa taji hilo. Mara ya mwisho ilikuwa mwaka 2007 wakati taji hilo liliponyakuliwa na Zhang Zilin.

No comments:

Post a Comment