KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Saturday, August 24, 2013

FILAMU YA FOOLISH AGE YA LULU KUREKEBISHWA



BODI ya Ukaguzi wa Filamu na Michezo ya Kuigiza nchini imezuia kufanyika kwa uzinduzi wa filamu ya Foolish Age iliyochezwa na msanii Elizabeth Michael 'Lulu'.

Bodi imeikataa filamu hiyo iliyopangwa kuzinduliwa Agosti 30 mwaka huu katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam hadi irekebishwe.

Taarifa kutoka ndani ya bodi hiyo zimeeleza kuwa, filamu ya Foolish Age imezuiliwa kutokana na waigizaji walioshiriki kuicheza, kuvaa nguo fupi.

Bodi hiyo imeagiza kuwa, sehemu hizo zote zifutwe na kufanyiwa marekebisho na kupitiwa tena kabla ya kuzinduliwa kwake.

Kwa mujibu wa taarifa hizo, iwapo filamu hiyo haitarekebishwa na kufikia vigezo vya madaraja vilivyowekwa na bodi hiyo, haitaonyeshwa.

No comments:

Post a Comment