KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, July 6, 2017

MWANAMUZIKI MKONGWE SHAABAN DEDE AFARIKI DUNIA



MTUNZI na mwimbaji mahiri wa nyimbo za muziki wa dansi nchini, Shaaban Dede, amefariki dunia.

Dede amefariki dunia leo asubuhi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, Dar es Salaam, alikokuwa amelazwa wiki mbili zilizopita kutokana na ugonjwa wa kisukari.

Mwimbaji huyo nyota nchini, amefariki akiwa mwanamuziki wa bendi ya Msondo Ngoma, ambayo alijiunga nao miaka miwili iliyopita akitokea Mlimani Park Orchestra.

Meneja wa Msondo Ngoma, Saidi Kibiriti, amesema hadi sasa bado haijaeleweka mazishi ya mwanamuziki huyo yatafanyika lini.

"Ndio kwanza tumeanza kikao cha kujadili taratibu za msiba kwa hiyo bado hatujajua mazishi yatafanyika lini na wapi,"amesema Kibiriti.

Dede alianza kujipatia umaarufu wakati akiwa bendi ya Dodoma International kabla ya kuhamia Msondo Ngoma na baadaye DDC Mlimani Park


No comments:

Post a Comment