KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, February 23, 2015

YANGA CHEREKO, SIMBA YACHINJWA


TIMU ya soka ya Yanga  jana iliendelea kujizatiti kileleni mwa ligi kuu ya Tanzania Bara baada ya kuichapa Mbeya City mabao 3-1.

Katika mechi hiyo iliyochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine mjini Mbeya, mshambuliaji Simon Msuva, aliendelea kudhihirisha ukali wake wa kuzifumania nyavu baada ya kuifungia Yanga bao la kuongoza dakika ya 18. Bao hilo lilidumu hadi mapumziko.

Mrisho Ngasa aliiongezea Yanga bao la pili dakika ya 59 baada ya kuwahadaa mabeki  wa Mbeya City pamoja na kipa wao.

Mbeya City ilipata bao la kujifariji dakika ya 68 kupitia kwa Abdul Seif baada ya kuunganisha krosi kutoka kwa Deus Kaseke.

Yanga iliendelea kutandaza soka ya kuvutia na hatimaye kupata bao la tatu dakika ya 78 kupitia kwa Haruna Niyonzima.

Wakati huo huo, mambo yameendelea kuwa mabaya kwa Simba baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kutoka kwa Stand United ya Shinyanga

Bao pekee na la ushindi la Stand United lilifungwa na Abashim Chidvebede dakika ya 11, akiunganisha mpira wa kona uliopigwa na Abuu Ubwa.

No comments:

Post a Comment