KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, February 2, 2015

FRANCIS CHEKA AFUNGWA JELA


NA LATIFA GANZEL, MOROGORO,

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Morogoro, imemhukumu bondia nguli nchini, Francis  Cheka, kutumikia kifungo cha miaka mitatu jela, baada ya kumtia hatiani kwa kosa  la shambulio  na  kudhuru mwili.

Cheka alihukumiwa kifungo hicho jana baada ya Hakimu Mkazi, Said Msuya, kumtia hatiani kwa kosa la kumshambulia na kumdhuru mwili aliyekuwa  Meneja wa baa yake, Bahati Kabanda.

Kwa mujibu wa hati ya mashitaka, Cheka anadaiwa kutenda  kosa  hilo  Julai  2,  mwaka  jana,  katika  eneo  la kata  ya  Uwanja  wa Taifa,  Manispaa  ya Morogoro.

Bondia huyo anadaiwa   kumpiga aliyekuwa  meneja wa  baa   yake   ilijulikanayo   kwa  jina  la  Vijana Social Hall  na kusababisha  kumdhuru sehemu mbalimbali za   mwili.

Akisoma hukumu hiyo, Hakima  Msuya alisema mshitakiwa atatumikia kifungo cha miaka mitatu jela na baada ya kumaliza kutumikia adhabu hiyo,  atatakiwa  kumlipa mlalamikaji gharama ya sh. milioni moja ya matibabu alizojitibia  baada  ya kupigwa  na  bondia huyo.

Akizungumza baada ya kupewa adhabu hiyo, Cheka alidai  kuna mkono wa   watu  wenye  lengo  la  kutaka  kuchafua  jina  lake   na maisha  yake .

Cheka alidai kushangazwa  kusomewa  kuwa  alikiri  kosa  la  kumpiga  mlalamikaji wakati  yeye  katika maelezo  yake  alikana shitaka.

"Ni  wazi kesi  yangu  ilipangwa  kuvurugwa  ili nifungwe na  kunipoteza  katika  ulimwengu wa  masumbwi," alidai.

Kocha wa bondia huyo, Abdallah  Komando, alidai  kuwa  kifungo cha  bondia  wake  kimemtia  simanzi  kubwa,   kwa kuwa kesi hiyo ingeweza kumalizika mezani.

Komando alisema kifungo cha bondia wake ni matokeo ya fitna za  kimichezo.

No comments:

Post a Comment