KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, February 12, 2015

BOBBI KRISTINA AFUNGUA MACHO


NEW YORK, Marekani

HALI ya mtayarishaji wa vipindi vya televisheni na mwanamuziki nchini Marekani, Bobbi Kristina Brown imeanza kutia matumaini.

Bobbi Kristina jana alifumbua macho, baada ya kulazwa kwa zaidi ya wiki moja kwenye chumba cha wagonjwa wenye uangalizi maalumu (ICU).

Taarifa hizo bila shaka ni njema kwa Wamarekani ambao kwa takribani wiki moja wako katika maombezi maalumu ya kumuombea nyota huyo ambaye ni mtoto wa nyota wa zamani wa muziki, Bobby Brown.

Kinda huyo alikutwa ameanguka bafuni na chanzo cha tukio hilo kinafanyiwa uchunguzi na Polisi nchini humo ingawa mumewe, Nick Gordon, anatajwa kuhusika.

Shangazi wa Bobbi, Leolah Brown, amethibitisha taarifa za maendeleo mazuri ya mgonjwa huyo ambaye aliyekuwa mahututi tangu Januari 31 mwaka huu.

Alisema jana alikwenda kumuona katika Hospitali ya Emory University ambapo Bobbi alifumbua macho kwa mara ya kwanza.

Leolah alisema hali yake inaridhisha na familia ina imani nduyu yao atapona ingawa bado wanaendelea na maombi.

“Bado tuna majonzi makubwa lakini, Bobbi anaendelea vizuri na hali yake inatia matumaini kuwa huenda akapona na kurejea katika hali ya kawaida,” alisema shangazi huyo.

Juzi familia ya Bobbi iliwataka madaktari kuzima mashine inayomsaidia kupumua ili aweze kufa katika tarehe kama marehemu mama yake Whitney Houston.

Whitney alifariki dunia Februari 11, 2012 baada ya kukutwa ameanguka bafuni katika Hoteli ya Beverly Hilton na pembeni kukiwa na pakiti za dawa za kulevya.

No comments:

Post a Comment