KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Saturday, November 24, 2012

UWANJA WA KAUNDA KUWA KAMA WA TAIFA





KLABU ya Yanga imetia saini mkataba wa awali wa kuanza kwa ujenzi wa Uwanja wa Kaunda uliopo mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam.
Mkataba huo ulitiwa saini jana makao makuu ya Yanga, kati ya Mwenyekiti wa klabu hiyo, Yusuf Manji na Kampuni ya Beijing Construction.
Akizngumza baada ya kutia saini mkataba huo, Manji alisema hatua hiyo ni mwanzo wa uongozi wake kutekeleza ahadi zake tangu ulipoingia madarakani Julai 15 mwaka huu.
"Leo tuna furaha kubwa kutia saini mkataba huu na wenzetu wa Beijing Construction ya China. Kamati ya utendaji tutahakikisha ujenzi unaanza kama
ilivyopangwa,"alisema.
Alisema taarifa za awali zimependekeza ujenzi wa uwanja huo kuanza baada ya miezi sita na kwamba uwanja huo utakuwa na uwezo wa kuchukua watazamaji kati ya 30,000 na 40,000 na utakuwa na hoteli.
Manji alisema baada ya ujenzi wa uwanja huo kukamilika, wataelekeza nguvu zao katika jengo lingine la klabu hiyo lililopo mtaa wa Mafia, Dar es Salaam.
Mwenyekiti huyo aliongeza kuwa, wanachama wanapaswa kufahamu kuwa,
uwanja huo hauwezi kujengwa na mtu mmoja kwa kuwa Yanga ni klabu yenye historia kubwa Afrika.
Kaimu Meneja wa Beijing Construction, David Zhong aliwataka wanachama na mashabiki wa Yanga watarajie ujenzi bora wa uwanja huo.
David alisema kampuni yake ina uzoefu wa kutosha katika masuala ya ujenzi na alitoa mfano wa ujenzi wa uwanja wa Taifa na Uhuru.


No comments:

Post a Comment