KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, November 15, 2012

KANSA INAVYOMMALIZA HALIMA


LAGOS, Nigeria
MWIGIZAJI Halima Abubakar wa Nigeria ameamua kupambana na ugonjwa wa kansa kwa kunyoa upara.
Halima ameamua kunyoa nywele zake katika maeneo yaliyoathirika kichwani kwake kutokana na ugonjwa huo.
Uamuzi huo wa Halima pia umelenga kutoa elimu kuhusu ugonjwa huo kwa watu wengine kwa kushirikiana na taasisi ya Wow Diva Organisation.
Takwimu za Nigeria zinaonyesha kuwa, ugonjwa wa kansa kwa sasa unaongoza kwa kuua watu wengi zaidi nchini humo kuliko ukimwi.
Kwa mujibu wa takwimu hizo, watu wengi wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na ugonjwa huo kwa sababu ya kutochukua tahadhari mapema kwa kupima afya zao.
Utafiti nchini humo umeonyesha kuwa, watu wengi wamekuwa wakiugua kansa ya titi, ngozi na utumbo na kupoteza maisha yao.

No comments:

Post a Comment