KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, November 22, 2012

POULSEN ATAMBA KILIMANJARO STARS IPO GADO

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya Tanzania Bara, Kim Poulsen ametamba kuwa, vijana wake wamejiandaa vyema kwa michuano ya Kombe la Chalenji, inayotarajiwa kuanza keshokutwa mjini Kampala, Uganda.
Poulsen alisema hayo leo wakati timu hiyo ilipofanya ziara katika Kiwanda cha Bia cha Mwanza (TBL) kwa ajili ya kujionea shughuli mbalimbali zinazofanywa na kiwanda hicho.
Kocha huyo kutoka Denmark alisema wamefanya mazoezi ya kutosha katika Jiji la Mwanza kwa vile hali ya hewa ya huko ni nzuri na inafafa na ile ya Kampala, ambako michuano hiyo itafanyika.
Poulsen apisema wamefarajika kuona kuwa mdhamini wao
anawathamini na kuwaalika kuona shughuli zinazofanywa kiwandani kwani wachezaji wameona na kujifunza mengi.
Nahodha wa timu hiyo, Juma Kaseja alisema wachezaji wote wako
katika hali nzuri na wamefurahia kuweka kambi Jijini Mwanza, ambako pia
walipata fursa ya kufanya ziara katika kiwanda cha TBL.
“Ziara kama hizi ni muhimu kwetu sisi kama wachezaji kwani
zinatusaidia kuelewa shughuli za mdhamini,” alisema.
Akizungumza mara baada ya ziara hiyo, Meneja wa Bia ya
Kilimanjaro Premium Lager, George Kavishe alisema hiyo ilikuwa njia
moja ya timu kupumzika kwani wachezaji waliweza kujionea shughuli
mbali mbali zinazofanywa na TBL.
“Pia ni njia moja ya kuileta timu karibu na watu kwani wachezaji
wamejumuika na wafanyakazi na kupiga nao picha za kumbukumbu,” alisema
na kuongeza kuwa wao kama wadhamini wataendelea kuipeleka timu kwa
watanzania ili waifahamu zaidi.
Wachezaji wa Kilimanjaro Stars pia walihudhuria semina maalumu iliyoandaliwa na Kilimanjaro Premium Lager na kusikiliza mada kadhaa.
Kilimanjaro Premium Lager imeanza kuidhamini timu ya Taifa kuanzia Mei mwaka huu kwa zaidi ya shilingi bilioni mbili kila mwaka kwa miaka mitano.
Udhamini huu pia unahusisha timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars.
Timu hiyo inatarajiwa kuondoka kesho kwenda Kampala kushiriki katika michuano hiyo.

No comments:

Post a Comment