KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, November 21, 2012

GAETANO KUPAMBA MISS EAST AFRICA 2012


MTANGAZAJI maarufu wa Kituo cha luninga cha Mnet cha Afrika Kusini, Gaetano Kagwa, anatarajiwa kuwa mshereheshaji katika sindano kubwa la urembo barani Afrika, Miss East Africa 2012.
Shindano hilo litafanyika Desemba 7, mwaka huu, katika Ukumbi wa Mlimani City ambapo, vinamwa wakali kutoka nchi za ukanda wa Afrika Mashariki na Kati pamoja na watatu kutoka Ulaya, watachuana kuwania taji hilo.
Taarifa ya waandaji wa shindano hilo, Kampuni ya Rena Events Ltd ya jijini Dar es Salaam, imesema kuwa Gaetano atasimama jukwaani kuongoza shindano hilo linalosubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki.
Rena imesema kuwa warembo wanachuana kuwania taji hilo wanaanza kuwasili jijini Dar es Salaam leo tayari kwa kuingia kambini kujiandaa na mpambano huo.
Mbali na warembo hao ambao tayari wameanza kuteka hisia za mashabiki wa fani ya urembo ndani na nje ya nchi, Gaetano ambaye ni raia wa Uganda pia anatarajiwa kupata mapokezi makubwa kutokana na mvuto wake tangu aliposhiriki shindano la Big Brother Afrika. Alijipatia umaarufu mkubwa ndani ya jumba hilo kutokana na kuwa na uhusiano wa kimapenzi na Abby.
Warembo watakaoshiriki shindano hilo ni kutoka nchi za Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Somalia, Djibouti, Eritrea, Sudan, Ethiopia, Malawi, Madagascar, Re-Union, Comoro, Seychelles na Mauritius. Wengine ni kutoka nchi tatu za Ulaya ambazo ni Ufaransa, Ubelgiji na Uholanzi.
Shindano hilo linatarajiwa kuonekana na mamilioni ya watu duniani, ambapo litarushwa kupitia luninga na kwa mtandao wa internet.

No comments:

Post a Comment