KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Saturday, November 24, 2012

NIYONZIMA ATOA MASHARTI MAGUMU KWA EL-MERREIKH




KIUNGO wa klabu ya Yanga, Haruna Niyonzima ametoa masharti magumu kwa klabu ya El-Merreikh ya Sudan, ambayo imewasilisha maombi ya kutaka kumsajili.

Akizungumza na Uhuru kwa njia ya simu kutoka Uganda, ambako timu yake ya taifa ya Rwanda, inashiriki kwenye michuano ya Kombe la Chalenji, Niyonzima alisema kwa sasa hana mpango wa kuihama Yanga.

Hata hivyo, Niyonzima alisema atakuwa tayari kujiunga na El-Merreikh iwapo itafikia makubaliano na Yanga na pia iwapo itatekeleza masharti yake.

"Kusema ukweli, kwa sasa sina taarifa rasmi za kutakiwa na El-Merreikh, lakini kama itakuwa hivyo, itabidi watekeleze masharti yangu,"alisema.

Aliyataja masharti hayo kuwa ni pamoja na kutokubali kufanyiwa majaribio kwa vile kwa kiwango chake, hastahili kufanyiwa majaribio na klabu yoyote ya Afrika.

Nahodha huyo wa zamani wa APR ya Rwanda aliyataja masharti mengine kuwa ni kulipwa mshahara wa kiwango chake, kupata maslahi bora na mazingira mazuri ya kufanyakazi.

Kiungo huyo alisisitiza kuwa, lengo lake kubwa ni kuendelea kuitumikia Yanga kwa vile alipoondoka Rwanda kuja nchini, aliweka dhamira hiyo.

Niyonzima ameelezea msimamo wake huo baada ya Katibu Mkuu wa Yanga, Lawrence Mwalusako kukaririwa wiki hii akisema kuwa, El-Merreikh imewasilisha maombi ya awali ya kutaka kumsajili mchezaji huyo.

Kwa mujibu wa Mwalusako, El-Merreikh inataka kumsajili Niyonzima kwa dola 100,000 za Marekani (zaidi ya sh. milioni 150), lakini Yanga inataka ilipwe dola 300,000 (sawa na zaidi ya sh. milioni 450).

No comments:

Post a Comment