KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, November 21, 2012

YVONNE:NASUBIRI KAULI YA IYANYA TU!



ACCRA, Ghana
MWIGIZAJI machachari wa Ghana, Yvonne Nelson amesema atakuwa tayari kufunga ndoa na mwanamuziki nyota wa nchi hiyo, Iyanya iwapo atakuwa tayari kufanya hivyo.
Gazeti la Yes la Ghana limemkariri mcheza filamu huyo akisema kuwa, anachosubiri ni kauli ya Iyanya iwapo atamtaka wafunge ndoa.
Yvonne ameelezea msimamo wake huo siku chache baada ya kukaririwa na vyombo vya habari akisema yupo pweke na anatafuta mwanaume wa kufunga naye ndoa.
"Inawezekana, huwezi kujua. Nitakubali kufunga naye ndoa iwapo ataomba iwe hivyo. Ni mtu mzuri na kijana mwenye mvuto,"alisema Yvonne.
Mahojiano kati ya Yvonne na gazeti la Yes yalikuwa kama ifuatavyo:
YES: Umeshampata mwanaume sahihi wa kufunga naye ndoa?
YVONNE: Sijampata, bado namtafuta.
YES: Unaweza kutueleza kuhusu uhusiano wako na Iyanya kwa sababu ametaja jina lako kwenye moja ya nyimbo zake?
YVONNE: Ni rafiki yangu mzuri. Ni shabiki wake mkubwa. Naupenda muziki wake. Ni mwanaume mwenye mvuto na wa aina yake. Huo ndio ukweli ulivyo.
YES: Iwapo atawasilisha ombi la kufunga ndoa na wewe leo, utakubali?
YVONNE: Inawezekana, ndio, inawezekana. Huwezi kujua. Nitakubali kama atawasilisha ombi hilo. Namaanisha ni mtu mzuri na mwenye mvuto.

No comments:

Post a Comment