KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Sunday, November 25, 2012

BOCCO AIBEBA KILIMANJARO STARS, YAITUNGUA SUDAN 2-0



Timu ya soka ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars leo imeanza vyema michuano ya soka ya Kombe la Chalenji baada ya kuichapa Sudan mabao 2-0 katika mechi iliyopigwa kwenye Uwanja wa Namboole mjini Kampala, Uganda.

Mshambuliaji John Bocco ndiye aliyeibeba Kilimanjaro Stars baada ya kuifungia mabao hayo mawili katika kipindi cha kwanza baada ya kuunganisha wavuni pasi maridhawa kutoka kwa Mrisho Ngasa.   Katika mechi nyingine ya kundi hilo iliyochezwa leo, Burundi imeipiga Somalia mabao  5-1 na hivyo kushika usukani wa kundi hilo kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa kati yake na Kilimanjaro Stars.   Michuano hio inatarajiwa kuendelea leo wakati Zanzibar itakapomenyana na  Eritrea.  

No comments:

Post a Comment