KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, November 22, 2012

ZANZIBAR HEROES YAAGWA, YAENDA UGANDA

Nahodha wa Timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes, Nadir Haroub Cannavaro akitoa shukurani kwa  Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo, Said Ali Mbarouk na kuahidi kuipeperusha vyema bendera ya Zanzibar katika michuano ya Chalenji itakayofanyika Uganda.
Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar(Zanzibar Heroes) Salum Bausi akizungumzia uimara ya timu yake ilivyojiandaa katika michuano hiyo ya Chalenji ilipokuwa ikiaga na Waziri wa Michezo Zanzibar.hafla hiyo imefanyika katika ukumbi mdogo wa hoteli ya bwawani. Zanzibar.
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo, Said Ali Mbarouk akizungumza na viongozi na wachezaji wa Timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) wakati wa kuikabidhi bendera na kuiaga katika ukumbi wa hoteli ya Bwawani, Zanzibar kwa ajili ya kuipeperusha katika michuano wa Kombe la Chalenji nchini Uganda,
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk (kushoto)akimkabidhi bendera nahodha wa timu ya Taifa ya Zanzibar Heroes, Nadir Haroub Canavarro. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa ZFATaifa, Alhaj Haji Ameir akishuhudia makabidhiano hayo yaliyofanyika katika ukumbi wa hoteli ya Bwawani Zanzibar. (PICHA ZOTE KWA HISANI YA ZANZINEWS)

No comments:

Post a Comment