KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, November 21, 2012

KILIMANJARO STARS EXTRA POWER, SAMATTA, ULIMWENGU NDANI



WACHEZAJI Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wamerejea nchini na kuongeza nguvu katika kikosi cha timu ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars kitakachoshiriki katika michuano ya Kombe la Chalenji.
Kilimanjaro Stars imeweka kambi yake jijini Mwanza kwa ajili ya kujiandaa kwa mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi keshokutwa mjini Kampala, Uganda.
Ofisa Habari wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Boniface Wambura alisema wachezaji hao wanaochezea klabu ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo, waliwasili mjini Dar es Salaam jana mchana wakitokea Congo kabla ya kwenda Mwanza.
Wambura alisema kurejea kwa wachezaji hao kumeifanya timu hiyo kukamilika katika idara zote na kuongeza kuwa, inatarajiwa kuondoka kesho kwenda Kampala.
Kwa mujibu wa Wambura, wachezaji hao wawili waliondoka nchini mara baada ya timu ya Taifa, Taifa Stars kumenyana na Kenya, Harambee Stars katika mechi iliyopigwa wiki iliyopita kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Kikosi cha Kilimanjaro Stars kipo chini ya Kocha Kim Poulsen na msaidizi wake, Sylivester Marsh. Wachezaji wanaounda timu hiyo ni makipa Juma Kaseja na Deogratius Mushi, mabeki Kevin Yondan, Erasto Nyoni, Issa Rashid, Shomari Kapombe na Amir Maftah.
Viungo ni Salum Abubakar, Amri Kiemba, Mwinyi Kazimoto, Ramadhani Singano, Mrisho Ngassa, Athuman Iddi , Frank Domayo na Shaaban Nditi wakati washambuliaji ni John Bocco, Simon Msuva, Christopher Edward, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu.

No comments:

Post a Comment