KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, November 21, 2012

JAMANI ACHENI KUNIFUATAFUATA, SIJAACHWA-INI EDO




LAGOS, Nigeria
MCHEZA filamu Ini Edo-Ehiagwina amekanusha madai kuwa, ameachana na mumewe, Phillip Ehiagwina.
Ini pia amekanusha madai kuwa, amepewa naira milioni 600 na Gavana wa Jimbo la Akwa, Godswill Akpabio ili ajenge chuo cha filamu katika mji wa Uyo.
"Kama ilivyo sheria kwangu, sina kawaida ya kujibu kila kinachozungumzwa ama kuripotiwa kuhusu mimi, lakini huu wa sasa ni wa kipumbavu na hauna maana,"alisema Ini alipozungumza na mtandao mmoja wa Nigeria wiki hii.
"Sielewi wanapata wapi taarifa hizi kwamba gavana wa jimbo langu amenipa naira milioni 600 kwa ajili ya kujenga chuo cha filamu Uyo. Hizi ni taarifa za uzushi, zinazotolewa na watu wenye kawaida ya kuwachafua watu maarufu,"alisema msanii huyo.
Ini alisema taarifa za kupewa pesa na gavana huyo kwa ajili ya kujenga chuo hicho ni za uzushi kwa vile hazina ukweli wowote.
Mwanadada huyo mwenye sura na umbo lenye mvuto alisema pia kuwa, haelewi ni kwa nini watu hao wameanza kumzushia uongo mwingine kwamba amepewa talaka na mumewe.
"Huu ni uongo mwingine, ambao unaweza kutolewa na watu wanaofurahia kuona ndoa za wenzao zikivunjika. Hakuna ugomvi wowote kati yetu na wala hatujatengana,"alisema.
Ini alisisitiza kuwa, bado yupo pamoja na mumewe na kwamba wanafurahia maisha wakiwa mume na mke.

No comments:

Post a Comment