KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Thursday, November 22, 2012

NYOTA WATANO WATEULIWA KUWANIA TUZO YA MWANASOKA BORA WA BBC 2012




Shirika la habari la BBC World Service, limetangaza orodha ya walioteuliwa kuwania taji ya mchezaji bora wa soka wa BBC mwaka wa 2012.
Wachezaji hao waliochaguliwa na wataalamu wa soka kutoka sehemu mbali mbali barani Afrika na kutangazwa rasmi na kipindi cha cha BBC world Service cha Newsday, inajumuisha wachezaji watano.Na ni pamoja na Demba Ba, kutoka Senegal wa klabu ya Newcastle ya England, Younes Belhanda wa Morocco anayeichezea klabu ya Montpellier ya Ufansa.
Mchezaji wa klabu ya Shanghai Shenhua, Didier Drogba kutoka Ivory Coast, Christopher Katongo wa Zambia akichezea klabu ya Henan Construction FC, inayoshiriki ligi kuu ya Uchina na Yaya Toure raia wa Ivory Coast na mcheza kiungo wa klabu ya Manchester City, ya England.
Orodha hiyo ilitangazwa na mtangazaji wa kipindi cha Runinga cha Focus on Africa, Peter Okwoche, na pia kuchapishwa kwenye mtandao na kupeperushwa moja kwa moja kupitia mtandao wa Internet wa idhaa mbali mbali za BBC, zikiwemo, Kifaransa, BBC Afrique, Maziwa makuu, inayotangaza kwa lugha ya Kinyarwanda na Kirundi, idhaa ya Hausa, Idhaa ya Kisomalia na Kiswahili ya BBC.
Mashambiki sasa wanaweza kupiga kura kupitia kwa mtandao wa Internet katika bbc.com/africanfootball na pia kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu ya mkononi ukitumia nambari +44 7786 20 50 75.
Ukitaka kumpigia kura Demba Ba, tuma nambari 1; kura ya Younes Belhanda andika nambari 2; na ikiwa unataka kumpigia kura Didier Drogba andika nambari 3; nambari 4 kumpigia Christopher Katongo na nambari 5 ukimtaka Yaya Touré.
Mhahariri wa Michezo wa idhaa ya lugha mbali mbali wa BBC David Stead, amesema orodha hiyo inatoa sura mpya kuhusu jinsi mchezo wa soka unavyoendelea kukua barani Afrika.
Kati ya walioteuliwa kuwania taji hilo mwaka uliopita, Yaya Toure pekee ndiye aliyefanikiwa kuteuliwa na hii ni kutokana na mafanikio yake msimu uliopita, ambapo aliisaidia klbau yake ya Manchester City kutwaa kombe la ligi kuu ya Premier kwa mara ya kwanza baada ya miaka 44.
Baada ya miaka kadhaa, hatimaye mchezaji kutoka Kaskazini mwa Afrika ni miongoni mwa wateule hao. Younes Belhanda, amekuwa nyota wa klabu ya Montpellier ambayo ilitwa kombe la ligi kuu ya Ufaransa.
Mashabiki wa Arsenal watafurahishwa na kujumuishwa kwa Demba Ba ambaye amejizatiti kuwa kuwa mchezaji nyota wa Newcastle na kufikia sasa tayari amfunga jumla la magoli manane kwenye ligi kuu ya Premier.
''Orodha hii pia imeangazia umuhimu wa ligi ya Uchina kwa wachezaji wa nchi za kiafrika, kama Drogba na Katongo. Drognba atapata uungwaji mkono na mashabiki wa Chelsea kutokana na bao la penalti alilofunga na kuisaidia kushinda kombe la klabu bingwa barani Ulaya naye Katongo, alipata umaarufu mkubwa baada ya kuiongoza Zambia kushinda kombe la Mataifa barani Afrika'' aliongeza Stead.
Shughuli ya kupiga kura inatarajiwa kumalizika saa tatu na nusu za Afrika Mashariki au saa mbili na nusu za Afrika ya Kati (18.30 GMT) wakati wa kipindi cha Focus on Africa siku ya Alhamisi tarehe 13 Desemba mwaka huu.
Mshindi wa tuzo hiyo ya mchezaji soka bora wa BBC mwaka wa 2012 atatangazwa tarehe 17 Desemba.
Sifa ya wachezaji hao na mafanikio yao kutokana na mechi zilizochezwa mwaka huu, yataangaziwa katika vipindi na lugha mbali mbali vya matangazo ya BBC.
*kumbuka wakati unapopiga kura kwa kutuma ujumbe mfupi wa simu ya mkononi, ada na malipo yanayohitajika kupeperusha ujumbe kimataifa zitatumika. Ujumbe mmoja tu utaruhusiwa kwa nambari moja ya Simu. Maelezo zaidi unaweza kuyapata kwenye mtandao bbc.com/africanfootball.

No comments:

Post a Comment