KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Wednesday, November 21, 2012

TUZO YA MWANASOKA BORA DES 30

KAMPUNI ya Wazalendo Bright Media imepanga kutoa tuzo kwa mwanasoka bora wa Tanzania katika hafla itakayofanyika Desemba 30 mwaka huu mjini Dar es Salaam.
Mratibu wa tuzo hiyo, Ahadi Kakore alisema mjini Dar es Salaam juzi kuwa, mchakato wa kuwapigia kura washindi wa tuzo hiyo ulianza tangu Agosti mwaka huu.
Kakore alisema washiriki wamekuwa wakipigiwa kura na mashabiki kupitia mitandao mbali mbali ya kijamii, facebook, twitter, blogu na simu za mkononi.
Alisema kwa sasa, kamati maalumu inayosimamia tuzo hizo, ipo kwenye mchakato wa kuchuja majina yaliyopendekezwa na mashabiki katika kuwania tuzo hiyo.
Kwa mujibu wa Kakore, hadi sasa mashabiki wamependekeza majina ya wanasoka 93, lakini kamati yake imepanga kuyachuja na kubaki 30.
"Tumepanga wachezaji wote watakaoingia fainali ya kuwania tuzo hiyo, washiriki kwenye semina maalumu ya uwekezaji na ujasiliamali ili waweze kujiandaa kwa maisha yao ya baadaye baada ya kustaafu soka,"alisema.
Kakore alisema semina hiyo imepangwa kufanyika Desemba 19 na 20 mwaka huu kwenye ukumbi wa hoteli ya Lamada, Dar es Salaam na itaendeshwa na wataalamu waliobobea katika masuala ya uchumi na fedha.
Mshindi wa tuzo hiyo atazawadiwa fedha taslimu, medali na cheti.

No comments:

Post a Comment