UWANJA wa Centenario wa Montevideo ndio uliotumika kwa fainali za kwanza za Kombe la Dunia zilizofanyika mwaka 1930 nchini Uruguay.
Katika fainali hizo, wenyeji Uruguay walitwaa ubingwa baada ya kuichapa Argentina mabao 4-2 katika mechi ya mwisho iliyohudhuriwa na watazamaji wapatao 100,000.
Jumla ya nchi 13 zilishiriki katika fainali hizo zilizochezwa kwenye viwanja vitatu tofauti katika mji wa Montevideo.
Wawakilishi wa Ulaya walikuwa wanne-Ufaransa, Yugoslavia, Romania na Ubelgiji, ambaowaliungana na nchi zingine nane kutoka Amerika ya Kusini na Marekani.Nchi nyingi kutoka barani Ulaya zilikataa kushiriki katika fainali hizo kwa madai kuwa, zilipewa taarifaya kushiriki katika muda mfupi wa siku 14 na zingine zilikuwa zikikabiliwa na ukata.
Romania ilifanikiwa kwenda Uruguay kutokana na ahadi ya Mfalme Karol kwamba,atawaruhusuwachezaji wa timu hiyo kupumzika kwa miezi mitatu na kuacha nafazi zao za kazi wazi hadiwatakaporejea kutoka kwenye fainali hizo.
Fainali za mwaka 1934 zilifanyika nchini Italia. Jumla ya nchi 16 zilishiriki kwenye fainali hizo, ikiwemo Misri iliyoliwakilisha bara la Afrika kwa mara ya kwanza.Michuano hiyo ilifanyika kwa siku 14 na wenyeji Italia walifanikiwa kutwaa ubingwa baada ya kuichapaCzechoslovakia mabao 2-1 katika mechi ya fainali.
Mshindi ilibidi apatikane katika muda wa nyongeza wa dakika 30 baada ya timu hizo kumaliza dakika 90 zikiwa suluhu.Katika mechi ya raundi ya kwanza, Italia ilipata ushindi mnono wa mabao 7-1 dhidi ya Marekani.Mmoja wa wachezaji wa Italia, waliong’ara katika michuano hiyo alikuwa Giuseppe Meazza.
Fainali za mwaka 1938 zilifanyika nchini Ufaransa na kwa mara nyingine, Italia ilitwaa ubingwa baada ya kuichapa Hungary mabao 4-2.
Mshambuliaji Giuseppe aliendelea kutawala vyombo vya habari baada ya kuifungia Italia bao la penalti katika mechi ya nusu fainali dhidi ya Brazil na kuiwezesha nchi yake kuibuka na ushindi wa mabao 2-1.
Baadhi ya matokeo ya kukumbukwa katika fainali hizo ni ushindi wa mabao 6-5 ilioupata Brazil
katika muda wa nyongeza dhidi ya Poland, ushindi wa mabao 4-2 ilioupata Uswisi dhidi ya Ujerumani na ushindi wa mabao 2-1 ilioupata Cuba dhidi ya Romania.
katika muda wa nyongeza dhidi ya Poland, ushindi wa mabao 4-2 ilioupata Uswisi dhidi ya Ujerumani na ushindi wa mabao 2-1 ilioupata Cuba dhidi ya Romania.
Fainali za mwaka 1950 zilifanyika nchini Brazil. Wenyeji walishindwa kuutumia vyema uwanja wao wa nyumbani baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Uruguay katika mechi ya fainali iliyochezwa mjini Rio de Janeiro.
Mshambuliaji Chiggia ndiye aliyeiwezesha Uruguay kutoka uwanjani kifua mbele baada ya
kuifungia bao la pili dakika 11 kabla ya mchezo kumalizika.India ilikuwa miongoni mwa nchi zilizofuzu kucheza fainali hizo, lakini ilijitoa baada ya Shirikisho la Soka la Dunia (FIFA), kuzuia wachezaji kucheza pekupeku. Inakadiriwa kuwa, watu 174,000walihudhuria mechi ya fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Macarana.
kuifungia bao la pili dakika 11 kabla ya mchezo kumalizika.India ilikuwa miongoni mwa nchi zilizofuzu kucheza fainali hizo, lakini ilijitoa baada ya Shirikisho la Soka la Dunia (FIFA), kuzuia wachezaji kucheza pekupeku. Inakadiriwa kuwa, watu 174,000walihudhuria mechi ya fainali iliyochezwa kwenye uwanja wa Macarana.
Ujerumani Magharibi ilitwaa kombe hilo kwa mara ya kwanza mwaka 1954 wakati fainali hizozilipofanyika nchini Uswisi. Ilitwaa ubingwa baada ya kuichapa Hungary mabao 3-2 katika mechi ya fainali.
Licha ya kufungwa katika mechi ya fainali, Hungary iliweka rekodi ya kusisimua. Iliianza
michuano hiyo kwa kuibamiza Ujerumani Mashariki mabao 8-3 katika raundi ya kwanza kabla ya kuzifunga Brazil na Uruguay katika mechi za robo fainali na nusu fainali.
michuano hiyo kwa kuibamiza Ujerumani Mashariki mabao 8-3 katika raundi ya kwanza kabla ya kuzifunga Brazil na Uruguay katika mechi za robo fainali na nusu fainali.
Kwa mara ya kwanza, wachezaji wa timu zote zilizoshiriki michuano hiyo walilazimika kuvaa jezizilizokuwa na namba. Jumla ya mabao 140 yalipachikwa wavuni katika mechi 26 za michuano hiyo.
Fainali za mwaka 1958 zilifanyika nchini Sweden. Katika michuano hiyo, Brazil iliweka rekodi ya kutwaa kombe hilo kwa mara ya kwanza baada ya kuwalaza wenyeji Sweden kwa mabao 5-2 katika mechi ya fainali.
Mshambuliaji Edson Arantes do Nascimento ‘Pele’ wa Brazil aliweka rekodi ya kuwa mchezaji
mwenye umri mdogo kucheza fainali hizo. Aliichezea Brazil akiwa na umri wa miaka 17.Pele, Garincha na Vava waling’ara kwenye kikosi cha Brazil na kuwavutia mashabiki wengi kutokana na staili yao ya uchezaji na ushambuliaji.
mwenye umri mdogo kucheza fainali hizo. Aliichezea Brazil akiwa na umri wa miaka 17.Pele, Garincha na Vava waling’ara kwenye kikosi cha Brazil na kuwavutia mashabiki wengi kutokana na staili yao ya uchezaji na ushambuliaji.
Katika michuano hiyo, mshambuliaji Just Fontaine wa Ufaransa aliibuka kuwa mfungaji bora baada ya kupachika wavuni mabao 13. Hadi sasa, rekodi ya Fontaine bado haijavunjwa.
Brazil ilitwaa tena kombe hilo mwaka 1962 wakati fainali hizo zilipofanyika nchni Chile. Katika mechi ya fainali, Brazil iliichapa Czechoslovakia mabao 3-1.Baadhi ya wanasoka wa Brazil waliong’ara katika fainali hizo ni pamoja na Pele, Garrincha, Vava, Didi na Mario Zagallo.
Pele hakuweza kumaliza michuano hiyo baada ya kuumia mguu katika mechi yaufunguzi.Katika fainali hizo, pambano kati ya Italia na Chile lilitawaliwa na vurugu nyingi. Wachezaji wawili wa
Italia walitolewa nje kwa kadi nyekundu, mmoja akiwa amevunjika pua baada ya kupigwa ngumi na mchezaji wa Chile, iliyoshika nafasi ya tatu baada ya kuichapa Yugoslavia bao 1-0.
Italia walitolewa nje kwa kadi nyekundu, mmoja akiwa amevunjika pua baada ya kupigwa ngumi na mchezaji wa Chile, iliyoshika nafasi ya tatu baada ya kuichapa Yugoslavia bao 1-0.
Fainali za mwaka 1966 zilifanyika nchini England na wenyeji walitwaa ubingwa baada ya kuishinda Ujerumani mabao 4-2 katika mechi ya mwisho.Mshambuliaji Geoff Hurst aliweka rekodi ya kuifungia England mabao matatu kati ya manne.Bao la pili la Hurst lilizua utata mkubwa kwa vile bado haijulikani iwapo mpira ulivuka mstari wa goli
baada ya kugonga mwamba wa juu. Ilibidi mwamuzi awasiliane na msaidizi wake kabla ya kuashiria kwamba lilikuwa bao halali.
baada ya kugonga mwamba wa juu. Ilibidi mwamuzi awasiliane na msaidizi wake kabla ya kuashiria kwamba lilikuwa bao halali.
Katika michuano hiyo, mshambuliaji Eusebio wa Ureno alifunga mabao
manane na kuiwezesha nchi yake kushika nafasi ya tatu. Matokeo yaliyowaduwaza mashabiki wengi ni ushindi wa bao 1-0 ilioupata Jamhuri ya Korea dhidi ya Italia.
manane na kuiwezesha nchi yake kushika nafasi ya tatu. Matokeo yaliyowaduwaza mashabiki wengi ni ushindi wa bao 1-0 ilioupata Jamhuri ya Korea dhidi ya Italia.
Brazil ilirejesha kombe hilo nyumbani mwaka 1970 baada ya kuichapa Italia mabao 4-1 katika mechi ya fainali, iliyochezwa kwenye uwanja wa Azteca uliopo mjini Mexico City nchini Mexico.
Michuano hiyo ilikuwa ya kwanza kuonyeshwa moja kwa moja kupitia kwenye televisheni, lakini picha zake hazikuwa za rangi.
Katika michuano hiyo, wachezaji Pele, Carlos Alberto, Jairzinho, Gerson, Rivelino na Tostao waling’ara na kutawala kwenye vyombo vya habari.Fainali hizo zitaendelea kukumbukwa kutokana na ushindani mkali uliojitokeza kwa timu shiriki na pia idadi kubwa ya mabao yaliyofungwa.
Mechi ya nusu fainali kati ya Italia na Ujerumani Magharibi ni mfano wa zile zilizokuwa na ushindani mkali. Baada ya dakika 90 kumalizika, timu hizo zilitoka sare ya bao 1-1. Dakika 30 zilizofuata, Italia ilishinda mabao 4-3. Mshambuliaji Gerd Muller wa Ujerumani Magharibi aliibuka mfungaji bora kwa kufunga mabao 10.
Ujerumani Magharibi ilitwaa kombe hilo kwa mara ya pili mwaka 1974 wakati fainali hizo zilipofanyika nchini humo. Ilitwaa ubingwa baada ya kuichapa Uholanzi mabao 2-1 katika mechi ya fainali iliyochezwa mjini Munich.
Uholanzi ilikuwa ya kwanza kupata bao lililofungwa kwa njia ya penalti na
Neeskens baada ya Hoeness kumchezea rafu Cruyff ndani ya eneo la hatari. Lakini jitihada za
Beckenbauer, Muller, Maier na Breitner ziliiwezesha Ujerumani Magharibi kusawazisha na kufunga bao la pili.
Neeskens baada ya Hoeness kumchezea rafu Cruyff ndani ya eneo la hatari. Lakini jitihada za
Beckenbauer, Muller, Maier na Breitner ziliiwezesha Ujerumani Magharibi kusawazisha na kufunga bao la pili.
Katika fainali za mwaka 1978 zilizofanyika nchini Argentina, wenyeji walifanikiwa kulibakisha kombe nyumbani baada ya kuichapa Uholanzi kwa penalti 3-1.Italia ilitwaa tena kombe hilo mwaka 1982 baada ya kuichapa Ujerumani Magharibi mabao 3-1. Paolo Rossi wa Italia aliibuka kuwa mfungaji borawa michuano hiyo baada ya kufunga mabao sita.
Katika michuano hiyo, Brazil ilionyesha soka ya kuvutia, lakini ilitolewa na Italia baada ya kuchapwa mabao 3-2 katika mechi ya raundi ya pili.
Argentina ilitwaa kombe hilo kwa mara ya pili mwaka 1986 wakati fainali hizo zilipofanyika nchini Mexico.Katika mechi ya fainali, Argentina iliichapa Ujerumani Magharibi mabao
3-2.Mshambuliaji Diego Maradona wa Argentina aling’ara katika fainali hizo kutokana na uwezo mkubwa aliouonyesha katika kupiga chenga, kukimbia na mpira kwa kasi na kufunga mabao.Ufaransa ilimaliza fainali hizo ikiwa ya tatu baada ya kuichapa Ubelgiji mabao 4-2. Morocco ilikuwa timu ya kwanza kutoka bara la Afrika kufuzu kucheza raundi ya pili ya michuano hiyo.Kombe hilo lilirejea tena Ujerumani Magharibi mwaka 1990 wakati fainali hizo zilipofanyika nchini Italia. Ilitwaa kombe hilo baada ya kuichapa Argentina bao 1-0 katika mechi ya fainali.
Cameroon iliweka rekodi ya kuwa timu ya kwanza kutoka Afrika kufuzu kucheza hatua ya robo fainali kabla ya kufungwa kufungwa na England. Mshambuliaji mkongwe Roger Milla wa Cameroon aling’ara katika michuano hiyo.
Katika michuano hiyo, mechi za nusu fainali kati ya Ujerumani Magharibi na England na kati yaArgentina na Italia ziliamriwa kwa njia ya penalti tano tano.
Mechi ya fainali mwaka 1994 ilikuwa ya kwanza kuamriwa kwa njia ya penalti tano tano. Katika mechi hiyo, Brazil iliishinda Italia kwa mikwaju 3-2 na kutwaa ubingwa.Awali, timu hizo zilitoka suluhu katika muda wa dakika 90 na 30 za nyongeza.
Italia ilipoteza penalti mbili zilizopigwa na Roberto Baggio na Franco Baresi.Ni katika michuano hiyo, mshambuliaji Maradona wa Argentina alifungiwa na FIFA baada ya kubainika
kuwa, alikuwa akitumia dawa za kuongeza nguvu.
Italia ilipoteza penalti mbili zilizopigwa na Roberto Baggio na Franco Baresi.Ni katika michuano hiyo, mshambuliaji Maradona wa Argentina alifungiwa na FIFA baada ya kubainika
kuwa, alikuwa akitumia dawa za kuongeza nguvu.
Ufaransa ilitwaa kombe hilo kwa mara ya kwanza mwaka 1998 baada ya kuichapa Brazil mabao 3-0 katika mechi ya fainali. Mabao mawili kati ya matatu ya Ufaransa yalipachikwa wavuni na mshambuliaji Zinedine Zidane. Bao lingine lilifungwa na Emmanuel Petit.
Mechi hiyo ya fainali ilikuwa na maluweluwe mengi kwa Brazil, hasa baada ya kocha Mario Zagallo kuamua kumchezesha mshambuliaji Ronaldo de Lima licha ya madaktari kueleza kwamba, hakuwa fiti. Davor Suker wa Croatia aliibuka mfungaji bora baada ya kufunga mabao sita.
Fainali za mwaka 2002 ziliandaliwa kwa pamoja na Japan na Korea Kusini. Brazil ilinyakua tena kombe hilo baada ya kuibwaga Ujerumani kwa mabao 2-0 katika mechi ya fainali. Mabao yote mawili ya Brazil yalifungwa na Ronaldo.
Italia ilinyakua tena kombe hilo mwaka 2006 baada ya kuichapa Ufaransa kwa penalti 5-3.
Mshindi ilibidi apatikane kwa njia ya penalti tano tano baada ya timu hizo kumaliza dakika 120 zikiwa sare ya bao 1-1.
Mshindi ilibidi apatikane kwa njia ya penalti tano tano baada ya timu hizo kumaliza dakika 120 zikiwa sare ya bao 1-1.
Hiyo ndiyo safari ndefu ya fainali za Kombe la Dunia kuanzia mwaka 1930 wakati zilipofanyika mjini Montevideo nchini Uruguay hadi mwaka 2006 zilipofanyika mjini Munich, Ujerumani.
NCHI ZILIZOTWAA KOMBE LA DUNIA 1930 HADI 2006
1930 Uruguay Uruguay vs Argentina 4-2
1934 Italia Italia vs Czechoslovakia 2-1
1938 Ufaransa Italia vs Hungary 4-2
1950 Brazil Uruguay vs Brazil 2-1
1954 Uswisi Ujerumani vs Hungary 3-2
1958 Sweden Brazil vs Sweden 5-2
1962 Chile Brazil vs Czechoslovakia 3-1
1966 England England vs Ujerumani 4-2 (pen)
1970 Mexico Brazil vs Italia 4-1
1974 Ujerumani Uholanzi vs Ujerumani 1-2
1978 Argentina Argentina vs Uholanzi 3-1 (penalti)
1982 Hispania Italia vs Ujerumani 3-1
1986 Mexico Argentina vs Ujerumani 3-2
1990 Italia Ujerumani vs Argentina 1-0
1994 Marekani Brazil vs Italia 3-2 (pen)
1998 Ufaransa Brazil vs Ufaransa 0-3
2002 Korea/Japan Ujerumani vs Brazil 0-2
2006 Ujerumani Italia vs Ufaransa 5-3 (pen)
No comments:
Post a Comment