KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, April 19, 2010

Hakuna uchaguzi mkuu mwaka huu-Sheikh Yahya Hussein



MTABIRI maarufu nchini, Sheikh Yahya Hussein ametoa utabiri mpya, ambapo safari hii amesema uchaguzi mkuu utakaowahusisha madiwani, wabunge na rais uliopangwa kufanyika Oktoba mwaka huu, hautafanyika.
Sheikh Yahya alitoa utabiri wake huo wiki hii kupitia kipindi chake maalum cha Nyota Zenu
kilichorushwa hewani na kituo cha televisheni cha Channel Ten.
Katika utabiri wake huo, mnajimu huyo maarufu katika ukanda wa Afrika Mashariki na Kati alisema, uchaguzi huo hautafanyika kutokana na sababu mbalimbali.
Hata hivyo, Sheikh Yahya hakuwa tayari kueleza sababu za kutofanyika kwa uchaguzi huo kwa madai kuwa, watu wanaweza kusema maneno mengi.
Utabiri huo mpya wa Sheikh Yahya umekuja siku chache baada hivi karibuni kutabiri kuwa, mtu
atakayejaribu kupingana na Rais Jakaya Kikwete kwenye kinyang’anyiro cha kuwania urais ndani ya CCM atakufa kifo cha ghafla.
Akifafanua kuhusu utabiri wake huo, Sheikh Yahya alisema kueleza sababu kwa lengo la kuondoa minong’ono baina ya Watanzania, ambao wamekuwa wakitumia muda mwingi kujadili utabiri wake na kuzua mijadala mizito miongoni mwa wanasiasa.
“Kama nilivyosema na kutabiri awali kwamba, atakayepingana na Kikwete atakufa ghafla basi sasa nasisitiza kwamba, uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu, hautafanyika na jamii itakuja kufahamu sababu zake hali ya mambo itakapojiri,” alisema Sheikh Yahya.

No comments:

Post a Comment