KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, April 19, 2010

RAY C APANIA KUTOKA KIVINGINE



SIKU chache baada ya kuwepo na malalamiko kwamba mwili wake umekuwa tipwatipwa, msanii nyota wa muziki wa bongo fleva nchini, Rehema Chalamila ‘Ray C’ amesema amepania kurudi kwenye hadhi yake ya zamani.
Ray C alisema mjini Dar es Salaam wiki hii kuwa, kwa sasa anafanya maandalizi kabambe ya kurudi kwenye ulingo wa muziki akiwa na mwonekano mpya, tofauti na wa sasa.
Alikiri kuwa ni kweli mwili wake umekuwa tipwatipwa na kushindwa kufanya vitu vyake kisawasawa, ambavyo vilimfanya atambe kimuziki mwanzoni mwa miaka ya 2000.
Malalamiko dhidi ya Ray C yalitolewa na mashabiki waliohudhuria onyesho la uzinduzi wa kampeni za kupambana na Malaria, lililofanyika hivi karibuni kwenye viwanja vya Leaders, Kinondoni, Dar es Salaam.
Katika onyesho hilo, Ray C alishindwa kulimiliki jukwaa kisawasawa kutokana na kuwa mzito katika kucheza, tofauti na alivyokuwa miaka ya nyuma.
“Hilo sasa halitakuwepo tena, nawaahidi mashabiki wangu kwamba wajiandae kumuona Ray C mpya na wasinishangae kwa jinsi nitakavyokuwa mwepesi,”alisema.
Katika hatua nyingine, Ray C amesema anafanya mipango ya kuanzisha taasisi yake kwa ajili yakushughulikia masuala yanayohusu watoto yatima.
Ray C alisema taasisi yake hiyo pia itakuwa ikishughulikia watoto wagonjwa, ambao wanakosamatumaini na kujiona ni watu wa kufa kutokana na kukosa huduma muhimu.
Alipoulizwa kuhusu ujio wa albamu yake mpya, msanii huyo aliyekuwa mahiri katika unenguajialisema, anatarajia kuiingiza sokoni Mei mwaka huu.

No comments:

Post a Comment