KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, April 19, 2010

NAKAAYA: Siasa haitanikwamisha kimuziki


MSANII nyota wa muziki wa kizazi kipya, Nakaaya Sumari amesema uamuzi wake wa kujiingiza katika masuala ya siasa hauwezi kumfanya ashindwe kuendelea na kazi yake ya muziki.
Naakaya alisema hayo mwishoni mwa wiki iliyopita mjini Dar es Salaam, ikiwa ni siku chache baada ya kutangaza kujiunga na CHADEMA.Alisema uamuzi wake huo umelenga kuwahamasisha vijana kujitambua zaidi na pia kutetea haki zao za msingi na demokrasia kwa jumla.

Nakaaya amekuwa msanii wa kwanza wa muziki wa kizazi kipya nchini kujitosa katika masuala ya siasa. Wasanii wengi wa muziki huo wamekuwa wakivutiwa zaidi na CCM.

“Sina hofu kwamba kazi zangu zinaweza kushuka kiwango kutokana na uamuzi wangu wa kujiingiza kwenye siasa. Nina hakika nitaweza kuendesha shughuli za muziki na siasa bila kuwepo na athari yoyote,”alisema.

Alisema alikuwa na kiu ya kujiunga na chama cha siasa kwa muda mrefu na hatimaye ndoto zake hizo zimefanikiwa baada ya kujitosa CHADEMA.
“Napenda wasanii wenzangu na watanzania kwa ujumla waelewe kwamba, uamuzi wangu huu
umelenga kuwahamasisha vijana kujitambua na kutetea haki zao za msingi, hasa kwa demokrasia bila kununuliwa ama kushurutishwa na vyama,” alisema Nakaaya.
Kufuatia uamuzi wake huo, CHADEMA imemruhusu msanii huyo kugombea nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama hicho baada ya kutimiza masharti na taratibu muhimu.

No comments:

Post a Comment