KWA HABARI ZA MICHEZO NA BURUDANI WASILIANA NASI KWA NAMBA 0719-153800 AU 0788-455808 AU EMAIL rashidzahor67@gmail.com '

Monday, April 19, 2010

NAOMI CAMPBELL:Sikufikiria ningetimiza miaka 40



LONDON, England“NIMEKUWA nikifanya kila ninaloweza kusahihisha maovu yote niliyowahi kuyafanya na siwezi kuwa mfungwa wa matendo yangu ya zamani. Siku zote nimekuwa nikijaribu kuwaheshimu watu,”anasema mwanamitindo maarufu duniani, Naomi Campbell.
Naomi alitoa kauli hiyo wiki hii alipokuwa akihojiwa na waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya
habari kuhusu mabadiliko yake kimaisha yake.
Mwanamitindo huyo amekumbana na mambo mengi katika maisha yake. Amewahi kufunguliwa kesi ya kumjeruhi kwa simu msaidizi wake na pia kutoa lugha chafu kwa wahudumu wa Shirika la Ndege la Uingereza.
Katika baadhi ya kesi, mwanamitindo huyo alihukumiwa adhabu ya kulipa faini na kufanyakazi za kijamii. Alitekeleza adhabu zote hizo.Naomi alifika kwenye chumba cha mkutano akiwa amechelewa kwa zaidi ya saa moja.
Pamoja na kuchelewa kwa muda mrefu, waandishi wa habari na wapiga picha waliendelea kumsubiri kwa hamu kubwa.Alianza kuwasili msemaji wake kisha akafuatia Naomi.
Mvao wake siku hiyo ulimfanya aonekane mwanamke mrembo na mwenye mvuto. Akiwa anatabasamu muda wote, mmoja wa waandishi hao anamtania kwa kumwambia kwamba uzuriwake unaweza kuwapagaisha watu.

Anabetua kichwa chake na kutoa kicheko kwa sauti.“Ninao watu walionizunguka, ambao wananiambia mimi ni mzuri. Lakini hilo linaingia kwenye sikiomoja na kutokea sikio lingine,” alisema mwanadada huyo.

Kuna mabadiliko makubwa katika maisha ya Naomi hivi sasa, kiasi kwamba Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela aliwahi kumtangaza kuwa mjukuu wake wa heshima.

Ikiwa imesalia miezi miwili kabla ya kutimiza miaka 40, Naomi bado anaonekana mrembo. Ngozi yakeni laini na nyororo na hana dalili yoyote ya kufanyiwa operesheni mwilini mwake.
Naomi, ambaye anatarajia kutimiza umri huo Mei 22 mwaka huu, alisema: “Nilifikiri kamwenisingeweza kutimiza umri huo. Ilifika wakati ilikuwa vigumu kwangu kujitazama kwenye kioo kwa sababu sikuupenda mwonekano wangu.”
“Kipindi cha kuanzia mwaka 1998 hadi 2005 kilikuwa kigumu kwangu. Nilipaswa kuyafanyiakazi
mambo muhimu, kile nilichokuwa nikihitaji kukifanyia mabadiliko na kile ambacho sikuwanikikifurahia,”alisema.
Mrembo huyo alisema hasira si kitu pekee, kilichokuwa kikimletea matatizo katika maisha yake.Alisema yapo mengine mengi na kuongeza kuwa, alilazimika kuhudhuria mafunzo maalum kwa ajili ya kudhibiti hasira zake.
“Kila mtu anaelewa maisha niliyopitia. Mimi ni binadamu, nafanya makosa, lakini nimejirekebisha. Siwezi kukanusha. Mengi yalinifedhehesha,”alisema.
“Sioni fahari kwa vitu nilivyovifanya na matukio yaliyotokea katika maisha yangu. Lakini nilifanya kitu fulani kwa ajili ya kujirekebisha,” aliongeza mwanamitindo huyo.
“Familia yangu na rafiki zangu wamenisaidia. Sipendi watu wanaosema ndio kwa kila kitu. Sitakikuzungukwa na watu wa ndio. Nafikiri ni watu hatari. Napenda watu wanaonieleza ukweli.Namuheshimu sana mtu, ambaye ananieleza ukweli moja kwa moja. Rafiki zangu wa kweli hunieleza kila kitu kama kilivyo. Nahitaji watu wa kunieleza hiki ni nini,”alisema.
Naomi alisema hawezi kujilaumu kwa vitu alivyovifanya katika maisha yake. Alisema anapaswakuwajibika kwa vitendo vyake. Lakini pia alisisitiza anao wajibu wa kujirekebisha.
“Kwa sasa nimepevuka.Nimechoshwa na maisha ya aina hii. Nataka kuishi maisha ya kawaida. Nataka kusahau yaliyopita. Umri unapoongezeka, maisha yako yanabadilika. Mambo unayoyapa kipaumbele unapokuwa na umri wa miaka 20 huwezi kuyapa uzito unapokaribia kutimiza miaka 40,”alisema.
Naomi alimshukuru Mandela kwa kuwa mstari wa mbele kumpa moyo kila alipokutana na matatizo. Alisema haelewi kwa nini Mandela ameamuakufanya hivyo.
“Kila wakati nilipofanya makosa, alinieleza nisivunjike moyo. Kila ninapopatwa na tatizo, huwanamuona mbele yangu. Kamwe hakuwahi kunikatisha tama,”alisema.
Matatizo aliyokumbana nayo Naomi katika maisha yake yalichangiwa kwa kiasi kikubwa na umaarufu wake, kabla hata hajajitosa katika fani ya mitindo ya mavazi.Marehemu Bob Marley aliwahi kumshirikisha mrembo huyo kwenye video ya wimbo wake wa ‘Is This
Love?’ akiwa na umri wa miaka saba. Miaka minne baadaye, alishiriki kucheza dansi katika video ya klabu ya Culture.
Akiwa na umri wa miaka 15, picha yake ilitumika kupamba jarida la Elle la Ufaransa na miaka miwili baadaye, aliweka historia ya kuwa mwanamitindo wa kwanza mweusi kupamba ukurasa wa mbele wa jarida la Vogue.
Baba wa mwanamitindo huyo, ambaye kamwe hakuwahi kumtangaza hadharani, alitengana na mama yake mzazi, Valeria miezi miwili baada ya kuzaliwa Naomi. Mama huyo alilazimika kuendesha maisha yake kwa kusafiri sehemu mbalimbali barani Ulaya, akiwa mcheza dansi na kumwacha Naomi akilelewa na mtumishi wa ndani. Uzuri wa sura yake, umbile lake na mwonekano wake vilibadili maisha yake kwa muda mfupi.
Miaka michache baadaye, alilipwa mamilioni ya pesa kutokana na kazi yake ya uanamitindo, akiwa na kinaKate Moss, Linda Evangelista, Christy Turlington, Cindy Crawford na Claudia Schiffer.
Naomi pia alishirikishwa kutengeneza video za nyimbo za wanamuziki mbalimbali maarufu duniani. Miongoni mwao wamo George Michael, Michael Jackson na wengine.Amewahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na wanaume mbalimbali kama vile Adam Clayton, Mike
Tyson, Sly Stallone, John F Kennedy Jr, Robert De Niro, Joaquín Cortés na Flavio Briatore. Kwa sasa, Naomi amekuwa akionekana mara kwa mara na mfanyabiashara bilionea wa Russia, Vladislav Doronin.

No comments:

Post a Comment